Home Kitaifa “Ligi kuu msimu huu usipime”- Sure Boy

“Ligi kuu msimu huu usipime”- Sure Boy

2726
0
SHARE

Kiungo wa Azam Abubakar Salum ‘Sure Boy’ amesema ligi kuu msimu huu ni ngumu kwa sababu timu za juu ya msimamo (Simba, Azam, Singida United, Mtibwa Sugar na Yanga) zinahitaji ubingwa hivyo kumekuwa na mchuano mkali.

Sure Boy mbaye alikuwa nje ya uwanja atarejea tena uwanjani kuisaidia timu yake katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara, amesema alikuwa nje ya uwanja kutokana na mambo binafsi ikiwemo msiba wa mama yake mzazi.

“Naendelea vizuri, nilikuwa nje ya uwanja kwa sababu ya msiba wa mama kwa hiyo nilikuwa namaliza mambo ya msiba. Nashukuru nimeshamaliza msiba kwa sasa najipanga ili niweze kucheza ligi, nilikuwa nafanya mazoezi mwenyewe kocha akaniita niende zanzibar kwenye fainali ya Mapinduzi Cup nimeungana na timu naendelea na mazoezi.

“Nimecheza mechi zote za ligi kuu msimu huu , mimi ni mchezaji wa muda mrefu kwenye ligi kwa hiyo kila msimu una changamoto zake inabidi ujiandae ili uweze kucheza uendelee kuwepo kwenye kikosi. Ligi ni ngumu kila timu imejiandaa, Simba wanaongoza, Azam nafasi ya pili, Singida wamekuja kwa hiyo ligi ni ngumu.

Kuhusu Azam kufanya vizuri kwenye michuano ya Mapinduzi na kutetea ubingwa wao, Sure Boy ameweka wazi siri ya mafanikio hayo: “Tunashirikiana ndio maana tumeweza kufanya vizuri, umoja ndio silaha ya yote haya.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here