Home Kitaifa Rekodi ya kocha mpya Mbeya City mmh!!…

Rekodi ya kocha mpya Mbeya City mmh!!…

3192
0
SHARE

Mbeya city ilivunja mkata na kocha wao aliyepita kinnah phiri raia wa Malawi kufuatia maelewano mabovu baina ya pande mbili yaliyosababishwa na kocha huyo kuidai klabu hiyo mishahara ya miezi kadhaa, baadaye timu hiyo ya ‘kizazi kipya’ iliingia mkataba wa mwaka mmoja na Nsanzurwimo Ramadhani kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.

Wakati Nsanzurwimo anaingia mktaba wa kuifundisha Mbeya City, timu ilikuwa kanda ya ziwa kwa ajili ya mechi zake za ligi,kwa mara ya kwanza akiwa jukwaani aliishuhudia timu yake mpya ikitoka sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Mwadui ugenini kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Mchezo wake wa kwanza kusimama kwenye benchi la ufundi la Mbeya City ilikuwa ni Oktoba 13, 2017 alipokiongoza kikosi chake kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba mwanza na kuambulia sare ya kufungana 2-2 alipokutana na kocha mburundi mwenzake Etine Ndayiragije.

Hadi sasa Januari 15, 2018 Nsanzurwim ameiongoza Mbeya City katika mechi nane (8) ya ligi kuu tanzania bara. Ameshinda mchezo mmoja tu (Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting), amepoteza mechi tano (5) na kutoka sare katika mechi mbili.

  • Mbao 2-2 Mbeya City
  • Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting
  • Azam 1-0 Mbeya City
  • Mbeya City 0-1 Simba
  • Yanga 5-0 Mbeya City
  • Singida United 2-1 Mbeya City
  • Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
  • Tanzania Prisons 3-2 Mbeya City

Kipigo kikubwa ambacho amekipata katika mechi hizo nane ni kile cha kufunga 5-0 alichopewa na Yanga Novembea 19, 2017 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Msimu uliopita Mbeya City walisubiri hadi mechi ya mwisho ili kujua hatma yao ya kubaki ligi kuu au kushuka daraja, msimu huu wakiwa wamesha cheza mechi 13 wapo katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 12 sawa na Kagera Sugar, Ndanda na Mwadui ambazo zimekaa juu ya Mbeya City kutokana wastani wao mzuri wa magoli.

City ipo nfasi ya tano kutoka chini juu ya majimaji yenye pointi 11, Ruvu Shooting ikiwa na pointi 11, Stand United yenye pointi 10 na Njombe Mji ambayo ina pointi nane.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here