Home Kitaifa Njombe Mji yavunja ukimya Sabasaba

Njombe Mji yavunja ukimya Sabasaba

2784
0
SHARE

Kama ulikuwa hujui basi chukua hii, leo Jumatatu Januari 15, 2018 Njombe Mji wameshinda kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani Sababa msimu huu (2017/18) baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Bao pekee la Njombe Mji limefungwa na Ditram Nchimbi kwa mkwaju wa penati kuipa ushindi wa kwanza timu hiyo ambayo imecheza mechi nane (8) katika uwanja wa nyumbani kati ya mechi 13 ambazo imeshacheza hadi sasa kwenye ligi.

Huo ni ushindi wa pili kwa Njombe Mji kwa mechi za ligi kati ya mechi 13 ambazo imesheza, imetoka sare katika mechi tano (5) na kupoteza michezo sita (6, imefikisha pointi 11 na kukaa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Matokeo ya mechi zote za Njombe Mji katika mechi za VPL

 • Njombe Mji 0-2 Tanzania Prisons
 • Njombe Mji 0-1 Yanga
 • Mbeya City 1-0 Njombe Mji
 • Majimaji 0-1 Njombe Mji
 • Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji
 • Njombe Mji 0-0 Lipuli
 • Simba 4-0 Njombe Mji
 • Njombe Mji 0-0 Stand United
 • Njombe Mji 0-0 Mbao
 • Njombe Mji 0-1 Azam
 • Ndanda 1-1 Njombe Mji
 • Njombe Mji 1-3 Singida United
 • Njombe Mji 1-0 Kagera Sugar

Njombe Mji ndiyo ilikuwa klabu pekee ambayo haikupata ushindi hadi kufikia mzunguko wa 12, hivyo imekuwa timu ya mwisho kupata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani huu na kufanya timu zote za VPL kuwa zimeonja ushindi wa ligi kwenye viwanja vyao vya nyumbani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here