Home Kitaifa Julio akubali ‘kiroho safi’ kichapo ligi daraja la kwanza

Julio akubali ‘kiroho safi’ kichapo ligi daraja la kwanza

5638
0
SHARE

Kocha wa Dodoma FC Jamhuri Kihwelu Julio’ amekubali ‘kiroho safi’ kwamba timu yake imepoteza mchezo wake dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kwenye mechi ya Kundi C ligi daraja la kwanza iliyochezwa uwanja wa Ali Hassani mwinyi Tabora.

Julio amekiri kwamba timu yake imepoteza mchezo dhidi ya Rhino kwa mabao safi ambayo hayakuwa na tatizo lolote baada ya kuzidiwa lakini akatoa dosari kuhusu uwanja.

“Mchezo ulikuwa mzuri Rhino walicheza vizuri wamepata nafasi wakazitumia vyema wametufunga magoli mawili, magoli safi wala hayana matatizo ni makosa ya safu yangu ya ulinzi wameruhusu magoli mawili.

“Mchezo wa soka ndio ulivyo huwezi ukawa unashinda kila siku, siku nyingine unafungwa.

“Mpira haukuwa na style kwa sababu ya uwanja ulivyo ndio maana walikuwa wanapiga na sisi tunapiga lakini wao mipira walliyopiga imekuwa na tija zaidi wamepata magoli lakini kiwanja hiki huwezi kucheza vile ambavyo unataka. Kwetu tulikuwa tunaweza kucheza na wao waliweza kucheza ingawa tuliwafunga lakini walicheza vizuri na leo wamecheza vizuri ingawa ilikuwa ‘power play’ lakini kwao ilikuwa na tija.

“Sina cha kuahidi, kufungwa ni sehemu ya mchezo kama vile watu wanavyokufa, kuna wengine walishakufa sisi tunaendelea kuishi lakini siku nyingine sisi tutakufa na wengine wataendelea kuishi ndio utaratibu.

“Kila kitu kinakwenda kwa zamu, mpira una matokeo matatu halafu hawa (Rhino) walikuwa wanacheza wakiwa na pointi 13 wangefungwa majaliwa yao ya kubaki daraja la kwanza yangekuwa magumu kwa hiyo lazima wacheze kwa nguvu ili waweze kujinusuru tena wamecheza kwao wamestahili kushinda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here