Home Kitaifa Waziri Ummy Mwalimu ni kicheko kwenda mbele Coastal Union

Waziri Ummy Mwalimu ni kicheko kwenda mbele Coastal Union

5756
0
SHARE

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewapa motisha wachezaji wa Coastal Union kiasi cha shilingi milioni mbili (2,000,0000) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwamba kila mechi watakayoshinda atatoa kiasi hicho kwa timu ili wachezaji wajitoe kuhakikisha timu yao inarudi ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

Waziri Ummy ametoa ‘mkwanja’ huo baada ya Coastal Union kushinda mechi yao ya ligi daraja la kwanza dhidi ya Mufindi United kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani na kujiweka katika nafasi nzuri ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.

“Maelekezo yangu kuhusu fedha hizi, nimeambiwa kuna watu 26 kwenye timu, kwa hiyo ningetamani kila mchezaji apate shilingi elfu hamsini (50,000) kama kifuta jasho. Siwapangii lakini kama wapo wachezaji 21 angalau basi kila mtu apate Tsh. 50,000 halafu inayobaki inaweza kuingia kwa mwalimu na watu wengine”.

“Lengo langu nikiwa kama mwanatanga na kiongozi kutoka mkoa wa Tanga, nataka kushirikiana na viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tanga lakini pia viongozi wa Coastal ilin kuhakikisha timu yetu inacheza ligi kuu. Bodaboda zitapata abiria, mama ntilie watauza lakini vijana hawa wanaocheza Coastal Union watakuwa na uhakika wa mishahara kwa mwaka mzima.”

Kundi A

  • Kiluvya United 1-3 Mgambo JKT
  • Mvuvumwa 0-3 JKT Tanzania

Kundi B

  • Coastal Union 3-0 Mufindi United
  • JKT Mlale1-0 Mawenzi Market
  • Mbeya Kwanza 0-0 KMC

Kundi C

  • Toto Africans 0-0 JKT Oljoro
  • Rhino Rangers 2-0 Dodoma FC
  • Biashara United 2-0 Alliance Schools

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here