Home Kimataifa Olunga kaweka rekodi isiyofutika La Liga

Olunga kaweka rekodi isiyofutika La Liga

10248
0
SHARE

Miaka mitatu iliyopita alikuwa tanzania na timu yake ya Gor Mahia iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kagame Cup ilikuwa ni mwaka 2015 ambapo aliisaidia klabu yake kucheza fainali na kupoteza kwa Azam ambao walitangazwa mabingwa wa michuano hiyo ambayo haijafanyika tena tangu mwaka huo, huyu si mwingine bali ni mshambuliaji mrefu raia wa Kenya Michael Olunga.

Olunga ameweka rekodi ya kuwa mkenya wa kwanza kufunga ha-trick kwenye ligi ya Hispania La Liga, aliingia akitokea kwenye benchi kuchukua nafasi ya Cristhian Stuani, aliingia wakati timu inaongoza kwa goli 1-0 akaisaidia kushinda kwa magoli 6-0 dhidi Las Palmas.

Licha ya kufunga magoli matatu, Olunga alitoa pasi ya mwisho ‘assist’ kwa hiyo amehusika katika magoli manne kati ya sita ambayo Girona wamefunga.

Hat-trick yake ilikuwa ya muda mfupi kwa wachezaji ambao wametokea benchi, alitumia dakika 22 kufunga magoli yote matatu, alifunga magoli yake dakika ya 57, 70 na 79.

Kwa sasa Olunga yupo Girona FC kwa mkopo akitokea China kwenye klabu ya Guizhou Zhicheng, hat-trick yake imemfanya ateke headlines za vyombo vya habari duniani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here