Home Kitaifa Mtibwa yaishusha Yanga

Mtibwa yaishusha Yanga

4161
0
SHARE

Klabu ya mtibwa sugar imepata ushindi wake wa sita kwenye ligi kuu tanzania bara kufuatia kuifunga lipuli kwa bao 1-0 ugenini na kukusanya pointi zote tatu.

Ushindi huo unaifanya mtibwa sugar kufikisha pointi 24 na kusogea kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya azam na simba kwa tofauti ya pointi mbili lakini mtibwa wo wako mbele kwa mchezo mmoja kwa sababu wameshacheza mechi 13 hadi sasa za mzunguko wa kwanza.

Bao pekee lililoihakikishia mtibwa pointi tatu limefungwa na hassani dilunga dakika ya 37 kipindi cha kwanza na kudumu kwa muda wote wa mchezo.

“Ushindi umekuwa faraja kwetu na kwa wapenzi wote wa klabu ya Mtibwa Sugarushindi ambao umetufanya tufikishe pointi 24 kutoka pointi 21 tulizokuwa nazo awali. Muunganiko ambao upo ndani ya mtibwa na wachezaji kutambua majukumu yao ndio siri ya ushindi huu”-Thobias Kifaru, afisa habari Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar imeziacha Yanga na Singida United ambazo zinabaki katika nafasi ya nne na tano katika msimamo wa ligi kabla ya mechi zao za mzunguko wa 13.

Matokeo mengine ya mechi za VPL zilizochezwa leo Januari 13, 2018

  • Stand United 1-0 Ruvu Shooting
  • Ndanda FC 1-1 Mbao FC

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here