Home Kimataifa Harry Kane avunja rekodi nyingine huku Real Madrid wakiendelea kuloa

Harry Kane avunja rekodi nyingine huku Real Madrid wakiendelea kuloa

5263
0
SHARE

Unaonekana huu ni muda wa Harry Kane na iko wazi kwamba kwa sasa Kane ndio namba 9 bora katika soka la sasa, hilo limedhihirika hii leo baada ya Muingereza huyo kupiga bao 2 wakati wakiiua Everton bao 4 kwa nunge.

Mabao mawili ya Kane yamemfanya kuwa mfungaji bora wa klabu ya Tottenham ambapo sasa Kane anakuwa amefikisha jumla ya mabao 98 katika michezo 135 na kumuacha Sheringham mwenye mabao 97 katika mechi 236.

Kwa matokeo ya leo Tottenham wamepunguza pengo la alama na Chelsea na sasa zinabaki alama 3 baada ya leo Chelsea kutoka suluhu ya bila kufungana na Leicester City matokeo yaliyowafanha kubaki na alama 47.

Wakati Kane akivunja rekodi hiyo, Real Madrid ambao wanatajwa kumtaka Harry Kane wamepoteza mchezo wao dhidi ya Villareal kwa bao moja kwa nunge na hii ikiwa mara yao ya kwanza kupoteza michezo miwili mfululizo tangu 2009.

Lakini hii leo ilikuwa raha na chungu kwa nyota wa Real Madrid CR7 kwani hii leo ulikuwa mchezo wake wa 500 tangu aanze soka la kulipwa na katika michezo hiyo sasa anakuwa amechezea vichapo mara 68.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here