Home Kitaifa Azam vs URA fainali ya mabingwa Mapinduzi Cup

Azam vs URA fainali ya mabingwa Mapinduzi Cup

5265
0
SHARE

Leo Jumamosi Januari 13, 2018 inachezwa fainali ya Mapinduzi Cup kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar kati ya Azam dhidi ya URA timu zote zikiwa zimetoka  kundi moja (Kundi A).

Mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye hatua ya makundi, ura iliifunga azam kwa bao 1-0, lakini ura haikuishia kuifunga azam pekee, simba walichezea kichapo kama cha azam katika hatua ya makundi pia kisha ura wakamalizia kwa yanga ambacho ni kigogo kingine cha tanzania kwa kuwatoa kwa mikwaju ya penati 5-4 kwenye mchezo wa nusu fainali.

Azam ndio wanaiwakilisha tanzania kwenye mchezo huo baada ya timu nyingine za bara na visiwani kutolewa katika hatua zilizopita. Haitakuwa mechi rahisi kwa azam kwa sababu Uganda wanaizidi tanzania katika mambo mengi ki soka, kuanzia ngazi za vilabu hadi timu za taifa.

Januari 14, 2016 URA walishinda taji la Mapinduzi Cup baada ya kuifunga Mtibwa Sugar 3-1 wakati huo Mtibwa ilikuwa chini ya kocha Mecky Maxime na wachezaji kama Shiza Kichuya said Mohamed ‘Nduda’ Salim Mbonde, Ally Shomari, Mzamiru Yassin Ibrahim Mohamed Mo, Ibrahim Jeba na wengine huku URA ikiongozwa na aliyekuwa nahodha wao Simeon Massa, Julius Ntambi, golikipa Bwete Brian, Peter Lwasa ambaye alifunga magoli mawili.

Kwa upande wa azam, wao ndio mabingwa watetezi waliotwaa taji hilo 2016/17 baada ya URA kuvuliwa ubingwa huo, kipindi hicho azam ilikuwa na nyota wengi ambao kwa sasa hawapo tena kwenye kikosi hicho. Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Yahaya Mohamed, John Bocco ambao kwa sasa hawapo  tena kwenye kikosi cha Azam kilichoshida ubingwa wa Mapinduzi msimu uliopita.

Azam ni wawakilishi wa ligi kuu Tanzania bara (ligi kuu ya Vodacom) wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakati URA wao wapo katika nafasi ya saba ya ligi kuu ya Uganda wakiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 15.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here