Home Ligi EPL Real Madrid zilipendwa kwenye soka la usajili….. Mabadiliko ya sera au ubahili...

Real Madrid zilipendwa kwenye soka la usajili….. Mabadiliko ya sera au ubahili kama Wenger

10087
0
SHARE

Rekodi za usajili zimevunjwa kwa mara kadhaa katika dirisha la usajili la kiangazi, lakini Real Madrid hawajaonyesha mshipa wa misuli ya utajiri wao kama ambavyo vilabu vingine vikubwa vilivyofanya.

Takwimu za matumizi ya fedha za usajili zinaonyesha mpaka sasa vilabu vikubwa 14 vimeshatumia kiasi cha 2.4 billions sawa na zaidi ya billioni ya 6 za kitanzania kwa ajili ya msimu huu tu, lakini Los Blancos wamehusika na matumizi ya 42.5 million euros katika kiasi cha jumla cha 2.4 Billions.

Hii sio kawaida ya Rais Florentino Perez ambaye huko nyuma alijenga sifa ya matumizi makubwa ya fedha katika usajili wa wachezaji kama Luis Figo, Zinedine Zidane, David Beckham, Ronaldo, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.

Real Madrid sasa wamekuwa wakisajili wachezaji wenye umri mdogo kwa bei nafuu, msimu huu wametumia fedha kumsajili Theo Hernandez na Dani Ceballos.

Kwa misimu miwili iliyopita Real Madrid wametengeneza kiasi cha €84m katika soko la usajili.

Kwa upande mwingine wapinzani wao FC Barcelona mpaka sasa wameshatumia kiasi cha 312.5m euros kuwasajili Paulinho, Ousmane Dembele na sasa Philippe Coutinho.

Vilabu vingine vikubwa vilivyotumia fedha nyingi kujimarisha ni Chelsea, Juventus, Liverpool, Atletico Madrid na vilabu vya jiji la Manchester – wametumia zaidi ya mara mbili ya kiasi walichotumia Los Blancos.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here