Home Kitaifa Pluijm anavyodhihirisha ubora wake

Pluijm anavyodhihirisha ubora wake

7134
0
SHARE

Kocha Hans van Pluijm ametudhihirishia kwa mara nyingine tena kwamba ni mwalimu mwenye uwezo mkubwa ambaye ana uzoefu wa soka la afrika na hasa soka la tanzania, namna alivyoweza kuwaunganisha akina kaseke, kambale, danny lyanga unaona kabisa singida uninvited ni ambayo imejiandaa na wachezaji wanacheza kwa kuonesha wanataka kitu.

Ukiangalia mchezaji mmoja mmoja unaona ni wachezaji wenye ushirikiano ndani ya timu na kinachowapa matokeo ni umoja uliopo na ile hali ya kutaka kuonesha watu wao ni miongoni mwa timu bora tanzania.

Ukiangalia mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo singida imeza kwa mara ya kwanza, ikiwa katika Kundi B pamoja na vilabu kama Yanga, Mlandege, JKU, Taifa ya Jang’ombe na Zimamoto, Singida United hakupoteza mchezo hata mmoja. Katika mechi tano ilizocheza katika hatua ya makundi ilishinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja (Singida united 1-1 Yanga). Walimaliza wakiwa vinara wa Kundi B wakiwa na pointi 13 sawa na yanga lakini wastani wao mzuri wa magoli uliwafanya wakae katika nafasi ya kwanza.

Imepoteza mchezo mmoja tu katika michuano ya Mapinduzi baada kukubali kufungwa goli 1-0 na Azam katika mchezo wa nusu fainali na safari yao ya Mapinduzi Cup kuishia hapo.

Katika mechi sita ambazo Singida United imecheza kwenye Mapinduzi Cup, imetoa mchezaji bora mechi ‘man of the match’ katika michezo mitano huku Shafiq Batambuze akitangazwa kuwa man of the match katika mechi nne kati ya sita, Deusi Kaseke ni mchezaji mwingine ambaye alitangazwa kuwa man of the match kutoka kaitka klabu hiyo.

Katika dirisha dogo la usajili Singida United walisajili wachezaji wengi lakini jambo la kupeneza waliwasajili vijana waliocheza fainali za afcon kwa vijana chini ya miaka 17. Danny Lyanga ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo, amefanya vizuri kwenye mashindano ya mapinduzi na kurudisha imani kwa kocha wake kwamba hajakosea kumsajili.

Kocha mkuu wa Singida United amesema mashidano ya Mapinduzi ni mazuri kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi lakini kutokana na ratiba yanasababisha wachezaji wanachoka kwa sababu wanacheza mechi nyingi mfululizo.

“Ni mashindano mazuri ambayo tumeyatumia kujiandaa kwa ajili ya ligi kuu lakini kwa sasa wachezaji wanachoka kwa sababu ya kucheza mechi nyingi mfululizo. Baada ya kutolewa kwenye mashindano tunaenda kujiandaa kwa ajili ya mechi yetu ya ligi dhidi ya Simba.”

Singida United itacheza dhidi ya Simba mchezo wa ligi kuu tanzania bara siku ya Alhamisi Januari 18, 2018 mchezo huo unatarajiwa kuwa wenye ushindani kutokana na nafasi ambazo vilabu vyote vipo. Simba wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya magoli watahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza ligi lakini kwa upande wa Singida United ambao wapo nafasi ya tatu wakiwana pointi 23 pointi tatu nyuma ya Simba na azam ambao ndio wapo juu ya msimamo wa VPL.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here