Home Kitaifa Mzee Dalali aionya Simba, la sivyo itakosa ubingwa

Mzee Dalali aionya Simba, la sivyo itakosa ubingwa

5983
0
SHARE

Mzee Hassan Dalali ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Simba amesema kama kuna mgogoro ndani ya klabu hiyo ni vyema ukatatuliwa mapema kabla hali haijawa mbaya isije kusababisha wakaukosa ubingwa ligi msimu huu.

“Inawezekana kuna matatizo simba, nimesoma kwenye gazeti nimeona wameandika simba kuna matatizo, kwa hiyo kama kuna matatizo mimi ningeushauri uongozi wa Simba wafanye kikao cha pamoja na vijana wetu maana ya timu halafu waangalie kuna tatizo gani ili waweze kutatua lile tatizo kwa sababu usipoziba uf a utajenga ukuta”-Dalali.

“Tukiacha kamgogoro haka kadogokadogo kanakwenda kanaendelea mwisho wa siku hata ubingwa tutaukosa halafu tutakuwa simba vipande vipande wakati nembo yetu sisi inasema nguvu moja, tuwe wamoja kama wazee wetu walivyotuachia tunazikana, tunauguzana, tunatembeleana, tunanaoleana yani simba ni baba mmoja mama mmoja.”

“Vizuri viongozi wa simba wakajitahidi kuondoa huo mgogoro na mgogoro utaondoka kwa vikao tu. Pande mbili zinazogombana basi wakae waweze kutatua kama wanaona kuna ugumu sisi wazee tupo watuite tusuluhishe tutawasaidia.”

Dalali amehoji iweje mchezaji anafanyiwa mabadiliko anasusa na kwenda kukaa jukwaani na mashabiki lakini pia hakufurahishwa na baadhi ya wachezaji kutopanda basi la timu baada ya timu kuwasili Dar ikitokea Zanzibar badala yake wakatawanyikia bandariki kila mmoja akitimka kivyake kwa usafiri anaoujua yeye wakati basi la timu lilikuwepo kwa ajili yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here