Home Kitaifa Muuaji Yanga ajazwa ‘minoti’

Muuaji Yanga ajazwa ‘minoti’

4145
0
SHARE

Kampuni inayoidhamini klabu ya mbao GF Trucks & equipment ltd imeongeza ‘mzigo’ kwa mshambuliaji wa Mbao Habib Kiyombo ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Disemba.

Kiyombo atachukua kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na tuzo kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo ambayo ni kampuni ya Vodacom hukui pia akipata king’amuzi kutoa kituo cha Azam TV ambacho ndio kituo chenye haki za kurusha live matangazo ya mechi za ligi kuu tanzania bara, lakini GF & Trucks wameamua kumuongezea mchezaji huyo kiasi cha shilingi laki tano (500,000).

Mkurugenzi wa GF & Trucks amesema wao kama wadhamini wa Mbao wameamua kutoa kiasi hicho kwa kiyombo ili kumpa changamoto yeye na wachezaji wengine wa timu hiyo kujituma na kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye mechi za ligi.

Kocha mkuu wa Mbao Etiene Ndayiragije amesema, anaamini Kiyombo na wachezaji wengine wa mbao wataendelea kujituma na kujitoa ili wafikie malengo yao.

“Ni motisha kwetu kwa sababu inatoa changamoto kwa vijana wetu na hata yeye anajua ni kazi kubwa amefanya hadi kufikia hapo kwa hiyo itamfanya apambane kwa juhudi na kujitoa zaidi lakini wengine wamepokea kwa furaha kwa sababu ni kazi ambayo ilifanyika ambayo wameiona na wao wanatamani siku moja kushinda tuzo hiyo.”

“Tunamuombea achukue tuzo nyingine nyingi zaidi isiwe hii tu ya mwezi Disemba, kama ameweza akapata hii anaweza kufanya vizuri na kufikia malengo yake.”

“Lazima niendelee kuwa nae karibu kumsaidia sio mazoezini tu lakini hata ajue anaenda wapi anafanya nini, kizuri kwake ni mchezaji mdogo halafu anajitambua anajua imetokea kwenye mazoezi ninaimani ataendelea kujituma na atafika mbali.”

Kwa mwezi Disemba ambao timu 12 kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo kila moja ilicheza mechi moja, Kiyombo aliisaidia timu yake kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Mbao ilishinda mabao 2-0.

Kiyombo aliwashinda mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 wa Simba dhidi ya Ndanda na beki Bruce Kangwa aliyeisaidia Azam katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here