Home Kitaifa ‘Mchawi mweusi’ bado haamini-amini kama anarudi VPL

‘Mchawi mweusi’ bado haamini-amini kama anarudi VPL

4475
0
SHARE

Licha ya kufikisha pointi 25 na kuongoza kundi la ligi daraja la kwanza, kocha wa JKT Tanzania Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ bado haamini kwamba wamepanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara pointi walizonazo huenda zikafikiwa na kuzidiwa na nyingine endapo zitafanya vizuri kwenye mechi zilizosalia za ligi daraja la kwanza.

“Tunachotaka sisi ni kutafuta pointi nyingi kadiri inavyowezekana tofauti na timu nyingine kwa hiyo kwa hiyo tunaamini tupate pointi nyingi tuendelee kuongoza ligi na penginepo tukapanda daraja. Kimsingi ni kwamba tuna pointi 25 lakini bado hazitoshi kupanda daraja”-Bakari Shime.

“Mashindano ni magumu timu ni nzuri zimekuwa zikibadilika mara kwa mara kwa maana kwamba mbinu za makocha na wachezaji kwa hiyo ni mashindano magumu mno huwezi ukabweteka ukaona kwamba unaongoza na utaongoza hadi mwisho wa ligi.”

JKT Tanzania inaongoza Kundi A ikiwa na pointi 25 kati ya timu nane za kundi hilo, timu inayoifuatia JKT Tanzania ni friend rangers ambayo ina popinti 19 huku timu zote zikiwa zimeshacheza michezo 10 hadi sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here