Home Kitaifa Golikipa wa Yanga anavyotamani kukutana na star wa Arsenal

Golikipa wa Yanga anavyotamani kukutana na star wa Arsenal

7192
0
SHARE

Golipa chipukizi wa yanga Ramadhani Kabwili amesema anatamani siku moja akutane na nyota wa Arsenal Mesut Ozil kwa sababu ndio mchezaji ambaye anamutia katika tasnia ya soka. Inaweza ikakushangaza Kabwili ni golikipa lakini anavutiwa na mchezaji wa ndani lakini ndio hivyo kila mtu ana sababu zake bila kujali nafasi aliyonayo kwa wakati huo.

Kabwili alisema anavutiwa na star huyo wa Arsenal na Ujerumani wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano na yahaya mohamed ‘mkazuzu’ alhamisi ya Januari 11, 2018 alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo alikuwa akitimiza miaka 18.

“Mesut ozil ni mchezaji wa kipekee halafu anajua mpira, anaivutia kwa style ya uchezaji wake natamani siku moja nimuone”- Kabwili.

Kila mchezaji anaechipukia ana ndoto za kucheza soka la kulipwa barani ulaya, kwa upande wa Kabwili yeye humwambii kitu kuhusu ligi ya Ufaransa na PSG.

“Napenda nipate fursa ya kwenda PSG Ufaransa, ni soka ambalo linanivutia sana, nikipata fursa ya kwenda Ufaransa naamini nitafanya vizuri zaidi kwa sababu ni kitu ambacho kipo moyoni kwangu.”

Kwa sasa Yanga inatoa nafasi kwa vijana wengi, Kabwili ametaja wachezaji ambao wanamvutia kwenye kikosi cha chao kwa wakati huu.

“Wapo wengi sana ila zaidi ni Yohana Nkomola na Juma Mahadhi.” Nkomola amesajiliwa yanga katika kipindi cha dirisha dogo lililopita lakini walicheza pamoja kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za AFCON  2017 kwa vijana chini ya miaka 17 .

Kabwili anapenda kuvaa kiatu kutoka kampuni ya Nike kwa sababu kina mfanya ajione yupo katika mwonekano mzuri.

“Napenda kuvaa kiatu cha kampuni ya nike namba 8.5 navutiwa nacho kwa hiyo ni kiatu ambacho nikivaa nakuwa katika mwonekano mzuri.”

Chelsea ndio klabu anayoishabikia kwa vilabu vya Ulaya: “Mimi ni shabiki wa chelsea, kwanza navutiwa na aina ya uchezaji wao pia sipati stress kama mashabiki wa Arsenal.”

Mbali na mchezo wa soka Kabwili anapenda basketball, akiwa mapumzikoni anapenda kusikiliza muzi anapenda nyimbo za Ali Kiba (seduce me), si mpenzi sana wa movies na anapenda. Kwa upande wa mambo ya misosi, jamaa anapenda sana kula wali kwa maharage.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here