Home Uncategorized RT yatoa ufafanuzi mgogoro kuhusu star wa riadha Tanzania

RT yatoa ufafanuzi mgogoro kuhusu star wa riadha Tanzania

2393
0
SHARE

Kuelekea kwenye mashindano ya Jumuia Madola mwezi April 2018 kumekuwepo na sintofahamu ya ushiriki wa mwanariadha Alphonce Simbu.

Mvutano uliopo ni kati ya serikali na ambayo inataka Simbu ashiriki mashindano ya Jumuia ya Madola wakati Chama cha Riadha Tazania (RT) wao hawataki Simbu ashiriki kwa sababu kuna mashindano mengine wanataka aende kushiriki Hispania lakini huko Jumuia ya Madola waende wanariadha wengine wenye sifa za kushiriki mashindano hayo.

Wilhem Gidabuday katibu wa chama cha riadha nchini amefafanua zaidi kwa nini wanamzuia Simbu asiende kushiriki mashindano ya Jumuia za Madola.

“Mashindano makubwa ya Olympic hatujawahi kupata medali ya dhahabu, watanzania wajiulize kwa nini hatujapata medali ya dhahabu ya mashindano makubwa hayo, kwa nini wimbo wetu wa taifa haujawahi kuimbwa kwenye mashindano hayo makubwa?”

“Mimi jibu ninalo, malumbano kama haya ya watu kushinikiza kwamba wadau wanataka hiki kama ni suala la wadau wadau wapo wazuri lakini vilevile wapo wadau wabaya. Viti vya uwanja wa taifa vinang’olewa na nani? Ni haohao wadau kwa hiyo watu waamini wapo wadau wazuri na wabaya.”

“Sisi kama chama tuna simama kimipango zaidi na si kihisia, kwa mawazo yangu kama msema kweli mnayenijua, mashindano ya Jumuiya za Madola ni ‘family games’  yani sisi tuliotawaliwa na muingereza tunaenda kumpigia makofi na kumshukuru kwa kututawala, sawa lakini kwa nini ushinikize mkimbiaji wetu bora aende?”

“Tanzania ya viwanda ya Magufuli haiangalii viwanda viwe kesho tu anataka viwanda vijengwe na ni mpango wa muda mrefu, ukiingilia taratibu zile lazima utapata matatizo, sisi mpango wetu ni kupata medali nyingi sio sasa hivi tu 2019, 2020 ndio lengo tunataka tuizawadie serikali ya awamu ya tano medali ya kwanza ya dhahabu ya Olympic Games hilo ni lengo.”

“Kwa hiyo Simbu anaweza asiende kwa sababu njema tu, na kama hatoenda kule basi atakwenda Vallencia ambayo ni mashindano ya dunia vilevile na ni half marathon ili aweze kwenda London ambapo vilevile kuna mkataba wake fulani ambao katika kupambana na wale adui watatu (ujinga, njaa na maradhi) Simbu atakuwa amekwepa ule umasikini ile fedha atakayopata Simbu itakuja kumwajiri mtu, italipa kodi.”

“Mimi nawasihi, Waziri wa michezo, Naibu Waziri wa michezo, Mkurugenzi na wote ambao wanapanga kwenda Australia waende tu safari njema lakini watuachie list tutawapa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here