Home Kimataifa Neymar atoswa kikosi bora cha UEFA, CR7 na Messi ndanii

Neymar atoswa kikosi bora cha UEFA, CR7 na Messi ndanii

6316
0
SHARE

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kikosi chao bora cha mwaka jana ambapo jina la mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar halipo kati majina 11 ya kikosi hicho.

Mlinda mlango katika kikosi hicho ni golikipa wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Gianluigi Buffon huku beki wa kulia ni Dani Alves anayekipiga PSG na kushoto ni Marcelo wa Real Madrid.

Walinzi wa kati ni nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akisaidiwa na mlinzi ambaye anatajwa kuwa katika rada za Manchester City na Chelsea Giorgio Chiellini.

Katika nafasi ya kiungo katika kikosi hicho wapo viungo wawili wa Real Madrid Luka Modric na Toni Kroos huku kiungo ambaye yuko katika kiwango cha hali ya juu na Manchester City Kelvin De Bruyne naye yupo.

Kwa upande wa washambuliaji kama kawaida washambuliaji wawili bora zaidi duniani Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo wapo katika kikosi hichi huku Eden Hazard wa Chelsea naye pia akitajwa na UEFA katika kikosi hiki.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here