Home Kimataifa Manchester United na City watunishiana misuli kwa Alexis Sanchez

Manchester United na City watunishiana misuli kwa Alexis Sanchez

6401
0
SHARE

Vita ya usajili wa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanche, imechukua sura mpya. Hapo mwanzo Man City walikuwa klabu pekee inayotajwa katika uhamisho huo lakini sasa Manchester United wameingia.

Inasemekana tayari United wameshatuma ofa kwa Arsenal kwa ajili ya Sanchez na watamtumia pia Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya manunuzi ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile.

Barcelona wanaonekana kutaka kukiimarisha sana kikosi chao kwani baada ya kumnunua Philippe Coutinho sasa miamba hiyo ya nchini Hispania inatajwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa Antoine Griezman toka Athletico Madrid.

Tayari kiungo mkabaji wa klabj ya Arsenal Francis Coquelin amemalizana na Valencia, Coquelin amejiunga na klabu hiyo ya nchini Hispania kwa mkataba wa miaka 4 uhamisho ulioigharimu Valencia £12m.

Florentino Perez raisi wa Real Madrid amejipanga kuwajibu Barcelona waliomnunua Philippe Coutinho, Perez anatajwa kupambana ili kumsaini mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah.

Inasemekana kwamba Lucas Moura amekubaki kujiunga na klabu ya Manchester United na sasa kinachosubiriwa kwa vilabu hivyo viwili ni kukubaliana ada ya uhamisho ambayo inatajwa kuwa £28m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here