Home Kitaifa URA wamemaliza vigogo wa VPL

URA wamemaliza vigogo wa VPL

2671
0
SHARE

URA imeziadabisha timu tatu za ligi kuu Tanzania bara hadi sasa kwenye kombe la Mapinduzi kwa kuzifunga timu hizo ambazo ambazo zipo katika nafasi za juu VPL.

Azam ndio walikuwa wa kwanza kuchezea kichapo toka kwa URA timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa Kundi A, Simba ikafuatia pia ikiwa ni mchezo wa Kundi A ambao ulikuwa ukiamua hatma ya timu hizo (URA na Simba) kwa sababu Simba ilikuwa ikihitaji ushindi wakati sare tu ingetosha kwa URA ambayo ilishinda kwa bao 1-0 na kuitoa Simba kwenye mashindano.

Balaa likahamia kwa Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ambapo pia nao wakachezea kipigo kwa mikwaju ya penati.

Yanga imeendeleza rekodi yake mbovu kwenye michuano ya mapinduzi cup baada ya leo januari 10, kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya URA kwa mikwaju ya penati 5-0 kufuatia suluhu ndani ya dakika 90 za mchezo huo.

Ni mara ya tatu mfululizo Yanga kupoteza mechi ya nusu fainali na kuaga mashindano ya Mapinduzi kwani mwaka 2016 na 2017 pia ilipoteza nusu fainali zake na kushia kuisikia fainali ya mapinduzi kwa muda mrefu.

Yanga wamepoteza nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo dhidi URA na mara zote wakitolewa kwa mikwaju ya penati, mwaka 2016 walitupwa nje ya mashindano kwa penati 4-3 baada ya sare ya kufungana 1-1.

  • 2016: ura 1-1 yanga (pt 4-3)
  • 2017: simba 0-0 yanga (pt 4-2)
  • 2018: ura 0-0 yanga (pt 5-4)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here