Home Kimataifa Rekodi ya Arsenal katika penati inasikitisha

Rekodi ya Arsenal katika penati inasikitisha

4833
0
SHARE

Mara ya mwisho ilikuwa tarehe 17 August 2013 ndipo Arsenal waliokoa mkwaju wa penati EPL, ilikiwa katika mchezo dhidi ya Aston Villa ambapo mlinda mlango Wojciech Szczensy aliokoa tuta la Christian Benteke.

Kuanzia wakati huo hafi sasa Arsenal kumepigwa matuta 23 kuelekea lango lao katika ligo kuu ya EPL lakini katika matuta yote hayo 23 hakuna hata tuta moja liliookolewa na hii ikiwa rekodi mbovu zaidi ya penati EPL.

Katika vilabu vilivyomaliza nafasi 6 za juu EPL msimu uliopita wanaofuatia kwa rekodi mbovu ya penati ni Chelsea ambao toka August 2013 wamepigiwa penati 11 huku kati ya hizo ni penati 1 tu iliokolewa.

Manchester United wako chini ya Chelsea kwani tangia kipindi ambacho Arsenal waliokoa penati, United walipigiwa jumla ya penati 16 ambapo kati ya penati hizo golikipa wao alifanikiwa kuokoa penati 3.

Tottenham wanafuatia ambao wenyewe katika kipindi hicho wamepigiwa penati 17 lakini wao wamefanikiwa kuokoa 5 huku Liverpool wakifuatia kwani wamepigiwa penati 18 na kati ya hizo golikipa wao aliokoa penati 7.

Manchester City hawako vibaya sana katika suala la kuokoa penati, City wamepigiwa jumla ya penati 12 lakini katika hizo walifungwa penati 7 tu huku penati 5 zilizobaki wakifanikiwa kuokoa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here