Home Kimataifa Lukaku akasirishwa na tuhuma za ushirikina, akimbilia mahakamani

Lukaku akasirishwa na tuhuma za ushirikina, akimbilia mahakamani

4456
0
SHARE

Habari kubwa duniani hii leo ni kumhusu Romelu Lukaku, mshambuliaji huyu wa United amekuwa habari kubwa baada ya moja ya wakurugenzi wa Everton kudai mwanasoka huyo alitumiwa ujumbe na mganga wa kienyeji ahame Everton.

Farhadi Moshiri alidai kwamba mshambuliaji huyo hakuondoka Everton kwa sababu za kifedha wala mshahara lakini Lukaku aliondoka Everton kwa sababu ya ushauri wa masuala ya kishirikina.

Habari hizi zimemfikia Romelu Lukaku na watu wake wa karibu wanasema amekasirishwa sana na jambo hilo, tayari Romelu Lukaku ameanza kutafuta ushauri wa kisheria ili kumchukulia hatua Moshiri.

Msemaji wa mshambuliaji huyo amesema kwamba Lukaku ni mtu wa dini na huwa hajihusishi kabisa na masuala yoyote ambayl hayahusiani na mungu ikiwemo masuala ya waganga wa kienyeji.

Akiendelea kusema kwamba Lukaku alihitaji kupata changamoto nyingine na pia hakuwa na imani na mkurugenzi huyo, sasa Lukaku tayari ameshaongea na timu yake ya kisheria tayari kumpeleka Morshidi mahakamani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here