Home Kitaifa Azam, URA, marudio fainali Mapinduzi Cup

Azam, URA, marudio fainali Mapinduzi Cup

3836
0
SHARE

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC wametinga fainali katika harakati za kulitetea taji lao baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa nusu fainali.

Azam wataiwakikisha Tanzania watakapocheza mechi ya fainali dhidi ya URA ya Uganda siku ya Jumamosi Januari 13, 2018, URA waliitoa Yanga kwenye mchezo wao wa nusu fainali uliopigwa kabla ya mchezo wa Azam vs Singida United.

Mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup URA vs Azam utakuwa ni kama marudio kwa sababu timu hizo zilipangwa pamoja Kundi A ambapo katika mechi iliyowakutanisha katika hatua ya makundi URA walishinda 1-0.

Kundi A lilikuwa na timu za URA, Azam, Simba, Mwenge na Jamhuri.

Bao la Azam limefungwa na Shaabani Idd Chilunda dakika ya 78 ikiwa ni dakika mbili tu tangu aingie akitokea benchi.

Katika mchezo huo, mchezaji Shafiq Batambuze wa Singida United alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kuzawadiwa king’amuzi cha Azam TV ambao ndio kituo chenye haki ya kuonesha ‘live’ mechi za Mapinduzi Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here