Home Kitaifa Vigogo wajitokeza mazishi ya Chama

Vigogo wajitokeza mazishi ya Chama

3770
0
SHARE

Wadau mbalimbali wa soka, wachezaji wa zamani, viongozi wa soka na wapenzi wa mpira wa miguu akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchema  wamejumuika pamoja katika mazishi ya aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa Athumani Juma Chama ‘Jogoo’.

Yaha Mohamed alifanikiwa kuzungumza na Abeid Mziba mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye aliezea kumbukumbu yake na marehem Chama hususan pale walipotaka kutoroka kwenda kucheza soka la kulipwa Uarabuni.

“Mwaka 1988 kuna klabu moja ya Oman walitufuata mimi na Chama, yeye alikuwa Dar es Salaam mimi niloikuwa Mbeya nikamuuliza Chama tunaondokaje akasema kwa kuwa yeyen hachezi sana (alikuwa ametoka kufanyiwa upasuaji) akasema nije kutoka Mbeya nimpitie Dar. Nilichokifanya nilipitia nyumbani kubadili nguo wakati huo Yanga ilikuwa inakwenda Mwanza kucheza dhidi ya Pamba mchezo wa ligi.”

“Nilimpitia Chama tukaenda kufanya mipango yetu ya kusafiri, jioni tukaanza safari mpaka Arusha, tulipofika Namanga habari zikawa zimeshafika pale kwamba kuna wachezaji wawili wa Yanga wanatoraka wanaenda kuhangaika na maisha mengine ya mpira Uarabuni. Tulikamatwa baada ya hapo Chama akaamua yeye anarudi mimi nikasema nakwenda mbele kwa mbele.”

“Nilivyofika Nairobi nikakutana na Muhando akaamua kunisaidia, ukaja ujumbe kwamba nisipewe visa anatakiwa arudi Tanzania ikabidi nirudi Yanga nikatulia. Baadae baada ya mwezi mmoja tukaondoka tena mimi na Chama (hatukufuata utaratibu maana tulinyang’anywa passport) ukapita Nairobi tukaenda hadi Muscut Oman tukawa tunaishi kwa kuchezea timu ya Oman.”

“Lakini tukiwa Oman tulitiliwa ugumu na chama cha soka wakati huo FAT, ikaja barua rasmi kwenye chama cha mpira cha Oman “Mziba na Chama hawana kibali cha kuchezea Oman” basi tukawa wachezaji wa mechi za kirafiki. Tulikaa mwaka mzima jamaa wakasema watupe uraia tukawaambia tunaenda nyumbani kujifikiria baada ya kuja huku nyumbani mimi nikaumia mguu na Chama akasema harudi tena na hapo ndio ikawa mwisho wa kucheza mpira akaanza shughuli za kibiashara.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here