Home Kimataifa Rekodi zinaonesha Jurgen Klopp atawafanya mumsahau Coutinho

Rekodi zinaonesha Jurgen Klopp atawafanya mumsahau Coutinho

5790
0
SHARE

Tayari Philippe Coutinho amesaini mkataba wa kuitumikia Barcelona hadi mwaka 2023 huku wiki 3 za mwanzo atakuwa nje kutokana na majeruhi, hii ni habari inayoumiza sana mashabiki wa Liverpool kwa sasa.

Lakini kwangu mimi Jurgen Klopp sidhani kama anaumia sana kuhusu hili la Coutinho, pamoja na kuwapa moyo toka dirisha lililopita la usajili lakini Klopp naamini alikuwa anafahamu kwamba Coutinho atauzwa.

Klopp ni kocha ambaye mara zote amekuwa haamini katika kubembeleza mchezaji, huwa ni kocha ambaye anawasikiliza wachezaji na kama mtu analazimisha kuondoka baasi lazima atamuuza bila uwoga.

Unakumbuka Roberto Lewandoski wakati Klopp yuko Dortmund? Lewandoski alikuwa wa motoo na ofa ya Bayern Munich ilipokuja na mchezaji akataka kusepa, Klopp hakuwa na ajizi alimuacha aende.

Na uzuri wa Klopp mara nyingi akiachia mchezaji mkubwa aondoke huwa analeta mwingine mwenye uwezo kasoro kuondoka kwa Lewandoski ambapo alikuja Ciro Imobbile akashindwa kutamba Dortmund.

Klopp huyu huyu alimuacha Nuri Sahin aliyeng’ang’aniza kwenda Real Madrid na akamuweka  Ikay Gundogan ambaye aliwasahaulisha mashabiki wa Dortmund kuhusu Sahin.

Vivyo hivyo kuondoka kwa Mario Gotze katika klabu ya Borussia Dortmund kuliwaliza sana mashabiki wengi wa klabu hiyo lakini ujio wa Mualmernia Henrikh Mkhitaryan kuliwafanya kusahau kuhusu Gotze.

Na pia usisahau kuwa kuondoka kwa Shinji Kafawa lilikuwa pigo sana kwa BvB na Klopp alikwenda kutafuta tu kijana mdogo aitwaye Marco Reus na akawafuta machozi tena mashabiki wa Dortmund.

Lakini safari hii presha ni kubwa sana kwa Klopp kwani ulimwengu mzima wanasubiri kuona nini anaweza kufanya na £142m, ukizingatia kwamba pesa za Suarez hazikuleta kilichotarajiwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here