Home Kitaifa JULIO ATAPIKA NYONGO: “Kuna watu labda wafe sisi ndio tutarudi Simba”

JULIO ATAPIKA NYONGO: “Kuna watu labda wafe sisi ndio tutarudi Simba”

17643
0
SHARE

Kocha wa Dodoma FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye ni kocha wa zamani wa Simba ametoa ya moyoni baada ya kuulizwa kuhusu tetesi zinazomhusisha kutakiwa na klabu yake ya zamani (Simba) kwa ajili ya kuinoa wakati huu ambapo klabu hiyo imemfukuza kocha mkuu kwa kigezo cha matokeo mabaya.

Katika maelezo ya Julioyanaonesha ni vigumu kwake kurudi kuifundisha Simba katika kipindi hiki, amezungumzia pia mazingira ya kufutwa kazi kwa Omog, hajamuacha kocha wa sasa Masoud Djuma lakini pia ametoa masharti kwa Simba ikiwa kweli wanahitaji aifundishe.

Kuhusu uwezekano way eye kurudi Simba    

“Hao wanaonihitaji mimi Simba labda wawe wamekufa kwa sababu Simba ni timu ambayo inawatu maalum ambao wanaweza kuwamudu kufanya wanachokitaka, watu wote wakweli na wenye uwezo hawatakiwi Simba kwa hiyo kuna watu labda wafe ndio sisi tutarudi Simba na watu hao wamekuja Simba sisi tumeanza kucheza mpira pale wao hawajaja lakini walivyopata madaraka wao wamekuwa na nguvu kuliko mtu yeyote na ndio wanaotuharibia Simba.”

Kufukuzwa kwa Omog

“Kila siku nimesema lakini wapenzi na wanachama wa Simba watakuja kunikubali hao watu wasiojua mpira ndio wanatufikisha hapa, kulikuwa hakuna sababu ya kumfukuza Omog mtu ambaye timu inafanya vizuri leo mnamleta mtu ambaye anabadilisha system timu inafungwa kipuuzi, haina morali, wachezaji hawana fitness ya kutosha.”

“Watu wote wanaoangalia kwenye TV pamoja na mimi naona kabisa kwamba kuna matatizo kwa hiyo watu wanatuharibia timu yetu sijui kwa nini hawaanzishi timu zao wanatukera sisi tuliopata vidonda kwa kuitumikia Simba.”

Omog aliwekewa mtego

“Suala la Omog kufukuzwa lilikuwa ni la muda mrefu hatma yake mmekiona, huwezi kumleta kocha msaidizi mwenye kiwango cha juu mfano mwenye leseni A umuweke na mwenye leseni A, haiwezekani lazima mmoja awe na leseni Amwingine ana B, leo wote wa juu walikuwa Simba inamaana kwamba walishamtengenezea Omog kitu cha kumfukuza ili baadae mwalimu aliyekuwepo achukue nafasi.”

Wachezaji

“Wachezaji wa Simba wanauwezo mkubwa sana wa kucheza mpira lakini watu wote wajiulize swali moja , Simba ya mwaka jana ambayo tumemaliza ligi mimi nilikuwa mmoja wa wa tu tuliokuwa tukifanya hamasa kwa wachezaji lakini jiulize swali kabla ya raundi ya pili kuanza ilikuwa inaongoza kwa tofauti ya point inane dhidi ya Yanga lakini kinyume chake Yanga wakawa mabingwa.”

“Ilikuwaje wakati tunaanza ligi Simba ikawa inaongoza lakini walipokuja kusajiliwa akina Kotei wenye uwezo mkubwa Simba ndio imeshuka na haikupata ubingwa, jiulize hapo kuna nini ndani yake.”

“Simba lazima wabadilike, inapofika wakati wa usajili waalimu ndio wasajili haiwezekani timu isajiliwe na watu wengine ambao uwezo hawana matokeo yake timu inakuwa namna hiyo, halafu wanakaa na chuki mimi nikiwa katika kufanya uhamasishaji ndani ya Simba kuna watu walikuwa wanasema Omog hafai afukuzwe mimi nilikuwa namtetea kwa kusema afukuzwe kwa sababu gani?”

Masoud Djuma

“Anachukuwa timu anabadilisha mfumo kwenye mashindano umeona wapi? Timu inatengenezewa mfumo wakati wa pre-season lakini Simba kila siku walimu wapya, ndio timu pekee iliyofukuza walimu wengi na mimi nasikia uchungu kusema Mungu analipa pengine kwa kutuonea mimi na King Kibaden kufukuzwa timu ikiwa nafasi ya tatu kwa sababu ya husda ya watu fulani.”

Masharti ya Julio kama Simba wanamtaka

“Kama wananitaka kwanza lazima niwe kocha mkuu kwa sababu vyeti vyangu vinaniruhusu, lapili hiyo nyuma wanayomlipia kocha huko Oysterbay nikakae mimi, nipewe gari na vitu endelevu kwa sababu ya class niliyonayo, huwezi kunirudisha pale niwe kocha msaidizi kwa yule mrundi ambaye naamini hawezi kunishinda kitu chochote.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here