Home Kimataifa Inter Millan, PSG, Madrid na Vasco Da Gama waumizwa na Philippe Coutinho

Inter Millan, PSG, Madrid na Vasco Da Gama waumizwa na Philippe Coutinho

9953
0
SHARE

Philippe Coutinho ni habari ya dunia, tayati amesaini mkataba wa kuitumikia Barcelona ambao wamekubali kutoa £145m kwa Liverpool, usajili wa Coutinho umewaumiza wengi na sio Liverpool tu bali hata wafuatao wameumia.

Inter Millan wanaweza kuwa kati ya klabu ambazo zimeumizwa na manunuzi ya Coutinho, Inter hawakuweka kipengele chochote katika mkataba wa Coutinho ambacho kinaweza kuwafaidisha akiuzwa na £145m walizokula Liva haziwahusu.

Sheria za FIFA za usajili zinatoa nafasi kwa timu iliyomlea mchezaji kupata walau 5% katika usajili wake lakini Liverpool walikuwa na Coutinho tangu akiwa na miaka 20 na hii inawasaidia kubaki na 100% yote hali ambayo inawafanya hata Vasco Da Gama waliomlea kuambulia patupu.

Baadhi ya vilabu kama United wana vipengele kwa wachezaji ambao wanauwauza ili wakiuzwa na vilabu vingine wafaidike, mfano Memphis Depay akiuzwa kwenda popote na Marseille kuna kiwango cha pesa ambacho United watapewa.

PSG nao wanalia kwani inasemekana wakati Neymar akisaini PSG moja kati ya wachezaji aliahidiwa kuletewa alikuwa ni Phellipe Coutinho lakini pamoja na kiasi kikubwa alichoahidiwa Coutinho aliikataa PSG.

Real Madrid walitaka kuleta ujanja ujanja kwa Coutinho, inasemekana masaa 12 kabla ya makubaliano kati ya Coutinho na Barcelona, Real Madrid walifanya jaribio la kumchukua Coutinho kutoka Barcelona.

Real Madrid walijaribu kutuma ofa karibia £170m kiasi ambacho ni kikubwa kuliko cha Barcelona lakini Coutinho tayari akili yake aliielekeza Barcelona na sasa ni mchezaji wa Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here