Home Kimataifa Arsenal na United vitani kumnasa mlinzi wa Chelsea

Arsenal na United vitani kumnasa mlinzi wa Chelsea

10282
0
SHARE

Vita ya usajili barani Ulaya ndio kwanzaa imepamba moto na watu wanapigana vikumbl sokoni na hizi ndio tetesi kubwa za usajili nchini Uingereza kwa masaa 24 yaliyopita.

Manchester United wanaweza kukabiliana na upinzani kutoka kwa Juventus katika kumnunua Mesut Ozil, inadaiwa kwamba miamba hiyo ya kutoka Italia nao wamepanga kutuma ofa kwa Arsenal kumtaka Ozil.

Habari kutoka nchini Ufaransa zinasema winga wa PSG Lucas Moura hayuko tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo na sasa Moura anataka kwenda kucheza EPL ambapo ni United anakodaiwa kwenda.

Arsenal na Manchester City wameingia vitani kumnunua mlinzi wa West Bromich Albion Jonnh Evans, Evans alikuwa akiichezea United na baadae aliuzwa kwenda WBA na sasa anaonekana kuwa kati ya walinzi bora PL.

Inaonekana Chelsea wanataka kuileta familia nzima ya wakina Hazard katika ligi ya EPL, kwani sasa klabu hiyo imehamisha nguvu zake kumnunua Thorgan Hazard ambaye anaichezea Borussia Monchenglabach kwa sasa.

Arsenal na Manchester United wanatajwa kuwa katika vita ya kumnunua mlinzi wa Chelsea David Luiz ambaye taratiibu ameanza kupoteza namba katika klabu ya Chelsea huku tetesi zikidai ana ugomvi na kocha Antonio Conte.

Inasemekana kwamba Ryad Mahrez yuko mbioni kujiunga na Liverpool, taarifa zinadai Leicester City wamekubali ofa ya £50m kutoka  kwa Liverpool na wakati wowote anaweza kwenda kujiunga nao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here