Home Kitaifa Yanga yaikwepa Azam Mapinduzi Cup

Yanga yaikwepa Azam Mapinduzi Cup

1994
0
SHARE

Baada ya sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Singida United, Yanga imebaki katika nafasi ya pili kutoka Kundi B kwenye Mapinduzi Cup ikiwa na pointi 13 ambazo ni sawa na Singida United vinara wa kundi hilo wakiongoza kutokana na wastani mzuri wa magoli.

Nafasi ya pili kwa Yanga kutoka Kundi B inamaanisha kwamba, watacheza dhidi ya URA katika mchezo wa nusu fainali URA ni vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 10 pointi moja mbele ya Azam ambao ni washindi wa pili wa kundi hilo kwa pointi zao tisa.

Singida United wakiwa wanaongoza Kundi B, watacheza nusu fainali dhidi ya Azam FC ambao ni washindi wa pili wa Kundi A.

Endapo Yanga wangeshinda mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Singida United wangefikisha pointi 15 ambazo zingewafanya kuongoza lao hivyo wangekutana na Azam kwenye mchezo wa nusu fainali.

Katika mchezo wa Yanga dhidi ya Singida United, timu ambazo zimekuwa na upinzani mkali kutokana na Singida kuchukua baadhi ya wachezaji ambao waliwahi kucheza Yanga ikiwa ni pamoja na kocha wao mkuu Hans van Pluijm, Danny Lyanga ndio alianza kufunga goli kwa upande wa Singida lakini bao hilo lilisawazishwa na Said Juma ‘Makapu’ dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Mechi za nusu fainali zitachezwa siku ya Jumatano Januari 10, 2018 katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar ambapo timu mbili zitakazoshinda kwenye  kila mchezo zitafuzu kucheza fainali ya Mapinduzi Cup 2017/2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here