Home Dauda TV Video: Yanga yaandaa mpango wa kuimaliza URA

Video: Yanga yaandaa mpango wa kuimaliza URA

4972
0
SHARE

Yanga itacheza dhidi ya URA mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2017/18 hiyo ni baada ya kutoka sare ya 1-1 na Singida United katika mchezo wa mwisho wa Kundi B ambao pia ulikuwa unaamua timu itakayoongoza kundi hilo.

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema, ndani ya siku mbili za mapumziko kabla ya mechi yao ya nusu fainali watakuwa wakijiandaa kwa ajili ya mchezo huo ili kuhakikisha wanashinda.

“URA ni timu nzuri na wamewafunga Azam na Simba timu ambazo ni nzuri, tumeshawaona wanavyocheza tuna siku mbili hizi za mapumziko tutajipanga na kujiandaa jinsi gani tuingie.”

Mechi za nusu fainali ya Mapinduzi Cup zitachezwa Jumatano Januari 10, 2018 ambapo timu mbili zitakazoshinda mechi za nusu fainali zitacheza fainali ya Mapinduzi Cup 2017/18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here