Home Dauda TV Video: Kocha wa Simba baada ya kutolewa Mapinduzi Cup

Video: Kocha wa Simba baada ya kutolewa Mapinduzi Cup

3539
0
SHARE

Simba imeondolewa kwenye michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kupoteza mchezo wake wa mwishi wa Kundi A kwa kufungwa 1-0 na URA ya Uganda, mchezo huo ulikuwa ni kama fainali kwa timu zote kwa sababu ndio ulikuwa uanaamua timu ambayo itafuzu kucheza nusu fainali. Simba ilihitaji pointi tatu wakati URA wao walikuwa wakihitaji sare tu ambayo ingewapa nafasi ya kusonga mbele.

Baada ya mchezo huo kumalizika, kocha wa Simba amezungumza na waandishi wa habari akieleza kilichosababisha wakapoteza mechi yao iliyopelekea kuondolewa kwenye mashindano katika hatua ya makundi huku mashabiki wakiwa na kumbukumbu ya timu yao kufika fainali katika msimu uliopita (2016/17).

“Mashabiki wanajua kwamba mwaka jana tulifika fainali kwa hiyo lazima mwaka huu tubebe kombe lakini wajue sio wao wanapanga matokeo, matokeo yanapangwa na Mungu. Vijana wamefanya kadiri walivyoweza lakinikwa nafasi tuliyofikia tunamshukuru Mungu, tunaenda kujiandaa kwa ajili ya ligi,”-Masoud Djuma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here