Home Dauda TV Iwe jua, iwe mvua, mnyama lazima kieleweke Mapinduzi

Iwe jua, iwe mvua, mnyama lazima kieleweke Mapinduzi

2153
0
SHARE

Kocha wa mkuu wa muda wa Simba Masoud Djuma amesema bado hawajakata tamaa yeye na vijana wake katika kutafuta nafasi ya kufuzu nusu fainali ya Mapinduzi Cup licha kupoteza mechi yao kwa kufungwa 1-0 na Azam.

Djuma amesema, watapambana hadi dakika ya mwisho  watakapokuwa wanacheza dhidi ya URA ili kuhakikisha wanafuzu kuungana na Azam ambao tayari wameshafuzu.

“Sisi hatujakata tamaa, tutapambana mpaka dakika ya mwisho tushindwe kama wanaume na tushinde kama wanaume na hicho tumeshazungumza na wachezaji kujitolea.”

“Timu ilikuwa ina siku nyingi haichezi na kufika kwenye eneo la 18 lakini sasa hivi tumekuwa tunafika kinachobakia ni utulivu na mawasiliano kwa hiyo tukifanikiwa katika hayo tutafanya vizuri kwa nguvu za Mungu.”

Kuhusu kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam kocha huyo raia wa Rwanda ametoa utetezi kwamba, Azam walikuwa wanahitaji sare tu katika mechi hiyo, hivyo mbinu yao ilikuwa ni kujilinda zaidi kitu ambaho hata wangecheza dhidi ya timu kubwa kiasi gani bado wangepata tabu.

“Walikuja kutafuta sare kwa hiyo walibaki nyuma sana, timu ikicheza vile hata icheze na timu kubwa kiasi gani itapata shida lakini ninachoshukuru licha ya kucheza vile lakini bado tulipata nafasi za kufunga hatukuzitumia ndio kile nilichokisema kwamba tunakuwa na wasiwasi mbele ya goli.”

Djuma amesema ni wiki mbili tu tangu aanze kupenyeza mifumo na mbinu zake lakini tayari ameanza kuona mabadiliko katika timu.

“Wiki mbili tu kwangu naona mafanikio makubwa, kuna wengine wanafanya kwa miezi mitano hadi sita lakini sisi wiki mbili tu unaona timu ina uwezo, inawezekana tusifanikiwe leo wala kesho lakini mabadiliko yanakuja na tutakuwa tunapata magoli mengi.”

“Nafurahi kuona watu wote wanatusapoti, nimekuwa nasoma mitandaoni, napata meseji nyingi za watu wanasema kazi inayofanyika sio mbaya na hicho ndio Simba ilikuwa inakosa, watu waendelee kutusapoti mazuri yanakawia lakini yanakuja.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here