Home Dauda TV Benchi la ufundi Simba lamvuruga Kichuya

Benchi la ufundi Simba lamvuruga Kichuya

7994
0
SHARE

Kama hukufuatilia game ya Simba dhidi ya UAR ambapo wenkundu wa Msimbazi walipoteza mechi hiyo kwa kufungwa 1-0, basi kuna jambo ambalo lilitokea na kuzua maswali mengi kwa wadau wa soka.

Benchi la ufundi la Simba lilifanya mabadilko kwa kuwatoa wacheza kadhaa ambao walianza kwenye kikosi cha kwanza na kuingia waliokuwa benchi, miongoni mwa wachezaji waliopumzishwa walikuwa ni Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Nicholas Gyan na Mzamiru Yassin.

Kitu kilichozua maswali mengi ni kwamba, Shiza Kichuya na Jonas Mkude hawakukaa kwenye benchi baada ya kutolewa ili kuwapisha wachezaji wengine, Kichuya alionesha wazi kutofurahishwa na maamuzi ya benchi la ufundi kumpumzisha wakati Mkude yeye alionekana akipiga story na baadhi ya wadau.

Afisa habari wa Simba Haji Manara alinaswa na kamera ya ShaffihDauda.co.tz akizungumza jambo na Kichuya ambapo inadhaniwa alikuwa akimtuliza mchezaji huyo kutokana na kuonesha wazi hakuridhia kupumzishwa.

Baada ya mechi, kocha wa Simba Masoud Djuma aliulizwa na waandishi kwa nini baadhi ya wachezaji wameonesha kutoridhishwa na uamuzi wa benchi la ufundi kuwafanyia mabaliko? Jibu la kocha huyo lilikuwa hivi: “Tumecheza mechi kwa tension kwamba lazima tufunge na lazima tushinde, kwa hiyo ule wasiwasi wa kutaka kufanya kitu vizuri unajikuta unaharibu lakini ndio game.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here