Home Kitaifa Yanga waitaka Simba nusu fainali Mapinduzi

Yanga waitaka Simba nusu fainali Mapinduzi

4831
0
SHARE

“Tuko hapa kwa ajili ya kucheza na timu yoyote ile, timu ambayo itakuwa mbele yetu tutacheza nayo na tutapata ushindi Mungu akijalia,” ni maneno ya kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa alipoulizwa endapo Yanga itakutana na Simba kwenye mechi ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup.

Baada ya Yanga kuifunga Zimamoto 1-0 kwenye mechi ya Kundi B, imefikisha pointi 12 sawa na Singida United lakini mabingwa hao watetezi wa VPL wanabaki nafasi ya pili huku Singida wakiongoza kundi hilo kwa wastani wa mabao.

Kesho Jumatatu Januari 8, 2018, Yanga itacheza dhidi ya Singida United mechi ambayo inasubiriwa kuamua nani kati yao ataongoza Kundi A na atacheza na timu gani katika hatua ya nusu fainali kutoka Kundi B.

Kuelekea mechi hiyo  Shadrack Nsajigwa amesema watacheza kwa kutafuta ushindi ndio maana katika mchezo wa leo dhidi ya Zimamoto kulikuwa na mabadiliko makubwa ya wachezaji, hiyo yote ni maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo ambayo wao wanaiona ni muhimu na wanaamini itakuwa ni mechi nzuri.

“Tunahitaji kushinda mchezo wetu wa kesho , hatuangalii nani tutacheza nae, kama tukishinda kesho lakini mpango wetu ni kushinda kwa hiyo litakalotokea.”

Ikiwa Yanga watashinda mechi ya kesho dhidi ya Singida United watamaliza hatua ya makundi wakiwa vinara wa Kundi B kwa kuwa watafikisha pointi 15 huku Singida ikibaki na pointi zake 12. Simba watacheza dhidi ya URA mchezo ambao pia utaamua ni timu ipi kati ya hizo itaungana na Azam kutoka Kundi A kucheza nusu fainali, Simba inahitaji ushindi tu dhidi ya URA ili ifikishe pointi saba na kufuzu kwa tofauti ya magoli dhidi ya URA ambayo pia ina pointi saba.

Endapo Yanga itaifunga Singida United na kuongoza Kundi B, kisha Simba ikashinda dhidi ya URA na kumaliza nafasi ya pili kutoka Kundi A, timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa nusu fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here