Home Kimataifa Huyu ndio mchezaji anongoza kuchezewa rafu EPL msimu huu

Huyu ndio mchezaji anongoza kuchezewa rafu EPL msimu huu

12783
0
SHARE

Pamoja na kwamba ameanza katika mechi chache EPL lakini kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ndio mchezaji ambaye katika ligi kui ya EPL katika msimu huu amechezewa rafu nyingi zaidi.

Wilshaire hadi sasa katika EPL ameanza katika mechi 11 tu lakini akiwa amechezewa rafu mara 14 , hadi sasa Wilshere ana wastani wa 3.59 kuchezewa rafu wastani ambao ndio mkubwa zaidi katika ligi kuu Uingereza.

Hali hii Wilshere ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akitumia muda mwingi nje ya uwanja inaleta mashaka kama ataendelea kuwa fiti hadi litakapofika kombe la dunia baadaye mwaka huu.

Anayefuatia kwa kuchezewa rafu EPL ni mshambuliaji wa Watford, japokuwa amecheza michezo mara mbili zaidi ya Wilshere (22) lakini ana wastani wa kuchezewa rafu wa 3.32 kwa kila mchezo.

Ashley Barnes yuko nafasi ya tatu katika orodha ya wanaopigwa sana viatu, mchezaji huyo wa Burnley hadi sasa ana wastani wa 3.31 katika michezo 21 huku Javier Hernandez “Chicharito” akifuatia nafasi ya 4.

Chicharito katika michezo 17 aliyoichezea West Ham ana wastani wa 3.27 na Eden Hazard wa Chelsea akishika nafasi ya 5 ambapo katika michezo 18 aliyoichezea Chelsea, Hazard ana wastani wa 3.08.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here