Home Kitaifa Ajibu nenda Ulaya kabla ya Maulana achana na chipsi

Ajibu nenda Ulaya kabla ya Maulana achana na chipsi

11291
0
SHARE

Priva ABIUD

Nmeona umri wa Ibrahim kwenye mitandao. Inasemekana ana miaka 21. Sawa haina tatizo. Ni umri sahihi kwa mwanasoka mwenye ndoto za kucheza ligi kubwa Ulaya. Sijui chochote kuhusu Ajib. Nimemuona mara kadhaa akicheza. Sio kwamba anajua sana. Ila ni mtu ambaye nina imani akipata nafasi hafanyi makosa. Ana mguu wenye ladha ya soka. Mguu wake una maelewano mazuri na mpira.

Kimsingi niseme kibongo-bongo basi nae anajua jua ila mimi naona bado sana. Siwezi kumfananisha na mshambuliaji yoyote Ulaya. Maana hafanani nao kabisa. Bado naona soka lake ni la kitanzania. Lakini umri wake na uwezo wake unafaa kwenda Ulaya.

Umri unamruhusu kujifunza lugha ya mpira wa Ulaya nae akawa kama wa Ulaya. Nataka nimwambie Ajibu kucheza Yanga na Simba si kitu. Utaishia kututishia kula chipsi mayai na kuendesha Brevis lakini kisoka tunakuona mwenzetu tu.

Ajib nataka nimwambie sisi tumewazidi Indonesia viwango vya FIFA. Indonesia wapo nafasi ya 162 huko sisi tupo ya 147. Tena wao walishawahi kushuka mpaka nafasi ya 191. Hawana ligi bora kama yetu. Ligi yao vurugu vurugu. Imeshabadilika kama mara 10. Zimewahi kutokea zaidi ya ligi 3 zote ndani ya taifa moja na zote zinaongoza kwa wakati mmoja. Hawajawahi kuwa na mchezaji mkubwa kama Samatta. Kwanza World Cup walienda mwaka 1938 baada ya Japan kujitoa.

Nimekwambia una mguu ambao unajua kuongea na mpira. Tatizo tu ni lugha ya mpira wetu na lugha ya mpira wa wenzetu hazifanani. Ndio maana sitaki nikufananishe hata na Dany Welbeck. Ajibu sio kama nakuponda nakueleza ukweli. Ukienda Old Trafford hata kubeba jezi huruhusiwi. Lakini mguu wako unaongea vizuri na mpira wetu wa bongo. Na nina imani umri wako na akili zako zinaweza kujifunza lugha za wenzetu kisoka na ukafanikiwa.

Simaanishi Kiingereza naamaanisha, kujituma, ubunifu, nidhamu, jitihada. Bro ukikaza unaweza kumkaribia Delle Alli hata robo. Nimekueleza kuhusu Indonesia, kuna dogo mmoja anaitwa Vikri Eggy Maulana. Huyu dogo anajua mpira nilipomuona niliacha kucheza mpira nikaamua kwenda kuuza mbege.

Mdogo wangu Ajib sikudharau. Nakueleza tu ukweli. Mbali na Indonesia kuwa na mfumo mbovu sana wa ligi, lakini leo Eggy Maulana anahitajika na Real Madrid, Espanyol na Benfica. Kwanza, yupo chuo hajacheza ligi yoyote zaidi tu ya kuchezea timu ya taifa ya Madogo. Sasa wewe Ajibu upo ligi kubwa huyu mwanafunzi ataendaje Ulaya kabla yako mzee baba?

Ajibu sitegemei uridhike na Passo au Vitz. Hata ukipata hela ya kupata chipsi miaka 10 usiridhike. Nataka uende Ulaya kabla ya Vikri. Nitashangaa soka lako linaaishia kuitwa mtani wa jadi. Kaza mwanangu. Mguu wako tayari umeshaongea na soka letu nenda nje sasa.

Achana na akina Manji, wala Mo asikurudishe Simba. We jamaa unajua. Unajua sana. Tatizo wachezaji wa bongo njaa na wengine wana akili mgando kama ya akina Eboue. Ajibu nenda Ulaya. Acha kukesha Insta piga tizi mzee baba. Ni hayo tu. Nenda kajaribu kuongea na mpira wa Ulaya kaka. Utanisamehe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here