Home Dauda TV Video: “Azam walinitoa thamani, namshukuru Pluijm”-Mudathir

Video: “Azam walinitoa thamani, namshukuru Pluijm”-Mudathir

7118
0
SHARE

Dauda TV imepiga exclusive story na kiungo wa Azam Mudathir Yahya anaecheza kwa mkopo Singida United ambayo imerejea tena ligi kuu Tanzania bara baada ya kusota kwa zaidi ya miaka 10 bila kucheza ligi hiyo.

Mudathir amefichua pia siri ya kukaa ‘mkeka’ kwa muda mrefu akiwa Azam hali iliyoanza kupoteza kipaji chake kwenye ramani ya soka, amemshukuru kocha wake wa  sasa Hans van Pluijm kwa kuona umuhimu wake na kumpa nafasi.

Siku za hivi karibuni Mudathir amekuwa kwenye kiwango bora na kuisaidia Singida United kuwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi November.

Kwa sasa Mudathir yupo Zanzibar na timu yake ya Singida United kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here