Home Kitaifa Simba vs Azam hii inaitwa lazima ukae

Simba vs Azam hii inaitwa lazima ukae

5447
0
SHARE

Leo Jumamosi January 6, 2018 kutakuwa na balaa pale kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, si kitu kingine ni pambano la Azam dhidi ya Simba mchezo wa Kundi A michuano ya Mapinduzi Cup 2017/18.

Kuna sababu tatu za msingi mechi hii kuwa ‘baab kubwa’ na kutolewa macho na timu zote mbili zitakapokutana majira ya saa 2:15 usiku.

Mechi inaamua hatma ya Azam Mapinduzi Cup 2017/18

Mechi hii ndio inaamua hatma ya Azam kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup, endapo watapoteza mchezo huo moja kwa moja safari yao itaishia hatua ya makundi, mchezo huu ni wa mwisho kwa upande wa Azam ambapo tayari wamecheza mechi tatu wakashinda mbili na kupoteza mchezo mmoja. Ushindi dhidi ya Simba utaifanya Azam ikate tiketi ya kucheza nusu fainali moja kwa moja kwa kufikisha pointi tisa. Kwa namna yoyo lazima watapambana ili kuhakikisha wanashinda na kufufuzu nusu fainali.

Simba wanaingia kucheza mechi hiyo ikiwa ni ya tatu kwao, walitoka sare mchezo wao wa kwanza   wakashinda mechi yao ya pili hivyo wana pointi nne katika kundi zinazowaweka nafasi ya tatu nyuma ya URA (vinara wa kundi wakiwa na pointi saba)  na Azam (nafasi ya pili wakiwa na pointi sita). Endapo Simba watapoteza mechi hiyo watasubiri hadi matokeo ya mechi za mwisho ambayo yataamua timu zinazosonga mbele.

Kisasi vs rekodi

Kama unakumbuka, Azam walitwaa ubingwa wa Mapinduzi msimu uliopita (2016/17) kwa kuifunga Simba 1-0 katika mchezo wa fainali, bao ambalo lilifungwa na Himid Mao na kuamua matokeo ya mchezo huo.

Kutokana na ushindani na upinzani uliopo kati ya vilabu hivi viwili, Simba itakuwa ikipambana kulipa kisasi cha kuchapwa na kushindwa kunyakua kombe la Mapinduzi mwaka uliopita wakati huo Azam watapambana kuhakikisha wanailinda rekodi yao kuifunga Simba kwenyen kombe la Mapinduzi kwa mara nyingine tena.

Erasto Nyoni, John Bocco vs Azam-Mapinduzi Cup

Mashindano ya Mapinduzi mwaka uliopita Erasto Nyoni, John Bocco na Aishi Manula na Shomari Kapombe walikuwa wachezaji wa Azam lakini wote hao kwa sasa ni wachezaji wa Simba baada ya kusajiliwa katika dirisha kubwa la usajili lililopita.

Nyoni na Bocco ndio wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Simba kinachoshiriki Mapinduzi Cup Zanzibar (Kapombe na Manula hawapo kwenye kikosi cha Simba kinachocheza Mapinduzi). Nyoni na Bocco safari hii watakuwa wakiitetea Simba dhidi ya timu kuhakikisha inapata ushindi na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Bocco ndiye nhodha mkuu wa Simba kwa sasa, wakati Azam ikishinda ubingwa wa Mapinduzi mwaka 2017 alikuwa ni nahodha wa Azam, anatafuta rekodi ya kushinda kombe hilo mara mbili mfululizo akiwa mchezaji wa vilabu viwili tofauti lakini akiwa nahodha wa vilabu hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here