Home Kitaifa Hivi unafahamu haya kuhusu John Bocco kabla ya Simba vs Azam?

Hivi unafahamu haya kuhusu John Bocco kabla ya Simba vs Azam?

7743
0
SHARE

Mshambuliaji wa Simba John Bocco anazidi kujitengenezea historia yake kwenye Mapinduzi Cup ambayo huenda ikawa ngumu kufikiwa na wachezaji wengine wazawa kwa kipindi cha hivi karibuni.

Inawezekana unajua mambo mengi makubwa ya Bocco, acahana na hayo hamia huku Mapinduzi Cup ambako kwa sasa ndio kumepamba moto zikipigwa mechi kuwania ubingwa huo.

Wakati hayo yakiendelea uanapaswa kujua haya macheche kuhusu John Bocco kuelekea mchezo muhimu wa leo Simba vs Azam (timu ya zamani ya Bocco).

John Bocco alishinda ubingwa wa Mapinduzi Cup 2016/17 akiwa nahodha wa Azam, aliiongoza Azam kufunga Simba 1-0 katika mechi ya fainali na kukabidhiwa ndoo ya Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein hiyo ilikuwa ni Januari 2017. Azam leo inacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi A, wakipoteza wanaaga mashindano wakishinda wanafuzu nusu fainali, John Bocco atawafungashia virago Azam?

Mashindano ya msimu huu (2017/2018) Bocco ni nahodha wa Simba baada ya Method Mwanjale aliyekuwa nahodha wa klabu hiyo kutemwa katika dirisha dogo la usajili. Katika mchezo wa leo dhidi ya Azam atacheza akiwa nahodha wa Simba kama alivyozoea kucheza akiwa nahodha wa Azam kwa miaka kadhaa iliyopita.

Bocco anakutana na Azam kwa mara ya pili akiwa mchezaji wa Simba, mara ya kwanza Bocco kucheza dhidi ya Azam tangu ajiunge na Simba ilikuwa ni Septemba 9, 2017 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa Azam Complex, mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya 0-0.

Endapo Simba itafanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi 2017/18 Bocco ataingia kwenye historia ya kuwa nahodha aliyetwaa taji hilo mara mbili mfululizo huku akiwa nahodha wa timu mbili tofauti (msimu uliopita 2016/17) Azam ilikuwa bingwa huku yeye akiwa nahodha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here