Home Kitaifa Hatma ya Simba mikononi kwa URA

Hatma ya Simba mikononi kwa URA

7671
0
SHARE

Simba imekubali kipigo kwa mara ya pili mfululizo kwenye kombe la Mapinduzi baada ya leo Januari 6, 2018 kuchapwa 1-0 ikiwa ni mchezo wa Kundi A, kabla ya mchezo wa leo Azam waliifunga Simba 1-0 kwenye fainali ya kombe hilo Januari 2017.

Azam inaongoza Kundi A kwa kufikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi nne, URA ina pointi saba katika nafasi ya pili, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne huku Mwenge na Jamhuri zenyewe zikiwa hazipo kwenye mbio za kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali.

Vita kubwa katika kundi hilo inabaki wa Simba na URA ambazo zote zina nafasi ya kusonga mbele kucheza nusu fainali ya Mapinduzi, timu hizo zitakutana katika mchezo wa mwisho ambao utaamua ni gani inaungana na Azam kutoka Kundi A kwenda kucheza nusu fainali.

Matumaini pekee ya Simba yapo kwenye mchezo wao dhidi ya Jamhuri, Simba inahitaji ushindi usiopungua magoli mawili ili kufuzu kwa wastani wa magoli, katika mechi zake mbili, Simba imefunga magoli matatu huku yenyewe ikifungwa mawili hivyo kufanya wastani wa magoli kuwa ni goli moja. URA inawastani wa magoli mawili kwa hiyo kama Simba itashinda mechi yake dhidi ya URA kwa tofauti ya magoli mawili itaungana na Azam kucheza.

Matokeo ya sare au kufungwa na URA yataifanya Simba kutupwa nje ya mashindano katika hatua ya makundi hivyo watakuwa wameondolewa katika taji jingine ndani ya siku 16 hiyo ni baada ya kutolewa katika kombe la Azam Sports Federation Cup December 22, 2017 kwa kufungwa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya kufungana 1-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here