Home Ligi EPL Virgil Van Djik ‘muosha masufuria anaeushangaza ulimwengu

Virgil Van Djik ‘muosha masufuria anaeushangaza ulimwengu

8662
0
SHARE

Safari ya mafanikio mara zote huwa ni ngumu sana, huwa sio rahisi kufikia kilele cha mafanikio kirahisi rahisi na hii ndio imemtokea pia mlinzi mpya wa Liverpool aliyenunuliwa toka Southamoton Virgil Van Djik.

Djik kwa sasa amekuwa habari kubwa ya dunia baada ya rekodi ya usajili aliyoweka, kwa sasa Van Djik ndio mlinzi ghali duniani akinunuliwa kwa £75m huku kwa mwaka akiweka kwenye account kiasi cha £10m.

Akiwa kijana mdogo wa miaka 16 Djik alikuwa hana kitu mfukoni na ilimfanya Djik kutafuta kazi ili kujiendeleza kimaisha na ndipo hapo aliamua kufanya kazi ya kuosha vyombo nchini kwao Uholanzi.

Katika mji anaotokea wa Brenda alifanya kazi hii kwa ujira mdogo sana huku wafanyakazi wenzake wakimuambia asahau kuhusu soka ni ngumu kutoka akiwa huko bali aendelee na kazi ya kuosha masufuria.

Djik hakutaka kusikia la mtu kwani aliamini soka ndio kitu chake cha kumtoa na sasa hadi mmiliki wa mgahawa ambao Djik alikuwa akifanyia kazi haamini kwamba mfanyakazi wake wa zamani amenunuliwa kiasi hicho.

Jacques Lips ambaye ni mmiliki wa mgahawa aliokiwa akifanya kazi Djik amesema aliposikia kiasi hicho cha pesa ilimbidi kurudia mara mbili mbili kutaja pesa hiyo kwani ni kiasi kikubwa mnoo cha pesa.

Jacques Lips akimuongelea Djik anasema “alikuwa anafanya kazi sana na pia alionekana kupenda sana mchezo wa soka, wakati mwingine nilimuambia achana na mambo yako ya soka endelea kuosha vyombo”.

Mmiliki huyo wa mgahawa anasema hawawezi kumsahau Djik kwani alikuwa mtu poa sana na hata namba yake ya simu ameiandika kwenye kitabu cha wafanyakazi na atampigia kumpa hongera.

Pamoja na mafanikio makubwa ambayo Djik ameyapata lakini mlinzi huyo hajasahau mji wao wa Breda na huwa anarudi kwenda kuwasalimia na kutoa shukurani kwa makocha na timu zilizomfungulia njia.

Kabla ya kutua Liverpool , Djik alicheza mtaani kwao Breda, kisha akajiunga na Willem ii baadaye akaenda FC Groningen zote za Uholanzi, kisha akanunuliwa Celtic waliomuuza Southampton na sasa Liverpool.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here