Home Ligi EPL Mashabiki wa Chelsea watofautiana kuhusu usajili wa Vidal

Mashabiki wa Chelsea watofautiana kuhusu usajili wa Vidal

13907
0
SHARE

Uhamisho wa Goretzka kwenda Bayern Munich umezidisha tetesi kwamba Artulo Vidal anaondoka Bayern Munich na wengi wanaona muelekeo wa Vidal ni EPL kwenda kujiunga na Chelsea.

Antonio Conte anaonekana kumhitaji sana Artulo Vidal kwani ni kocha ambaye anaonekana kutaka kuleta jeshi alilokuwa nalo Italia lije kufanya kazi EPL na Vidal anaonekana kweli amekaribia darajani.

Conte anataka kumuunganisha Vidal, Fabregas, Bakayoko na Kante kujaribu kutafuta utatu aliokuwa nao Juve ambao viungo watatu walikuwa wakimpa mabao 20/25 kwa msimu kitu ambacho Chelsea kinakosekana.

Lakini umri wa Vidal umeonekana kuleta mabishano makubwa mtandaoni, Vidal ana miaka 30 umri ambao unaonekana mkubwa kuja kupambana katika ligi ya EPL ligi yenye ushindani mkubwa sana.

Lakini hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Chelsea kununua wachezaji wenye umri mkubwa kwani walishamnunua Makelele akiwa na miaka 30, Ballack alikuwa na 29 huku Drogba naye alinunuliwa akiwa na 27.

Chelsea wanataka kutoa kiasi cha £33m kwa ajili ya kumsainisha Artulo Vidal lakini Bayern Munich wamekataa kiasi hicho cha pesa na wanataka zaidi ya £50m ili waweze kumuuza Vidal kwenda Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here