Home Ligi EPL Hizi hapa habari za Dyabala kutua United na nyingine za usajili

Hizi hapa habari za Dyabala kutua United na nyingine za usajili

17960
0
SHARE

Inasemekana klabu ya soka ya Juventus imekataa dau la £60m kutoka kwa Manchester United wanaotaka kumnunua Paulo Dyabala na sasa Juventus wamewaambia United wakaongeza pesa hiyo mara mbili ndio warudi tena.
Tetesi nyingine kuhusu Dyabala zinasema United wamejaribu kumtumia Mkhitaryan kama sehemu ya dili hilo lakini Juventus wameweka ngumu na kusisitiza kwamba wanataka pesa tu kwa Dyabala.

Chelsea hao hao wanaonekana kumganda mlinzi wa kushoto wa Juventus Alex Sandro ambaye katika dirisha kubwa lililopita la usajili walimkosa na sasa wamerudi tena na £50m kwa ajili ya kumnunua Sandro.

Kutokana na mashindano ya kombe la dunia yanayotarajia kutimua vumbi baadaye mwaka huu inadaiwa kwamba golikipa wa Manchester United Sergio Romero anataka kuondoka United ili kwenda kutafuta namba pengine.

Manchester United wanataka kumchukua Joao Mario kutoka Inter Milan kama sehemu ya mabadilishano na Henrikh Mkhitaryan ambaye anatajwa kuwa njiani kueleka Inter Milan katika msimu ujao wa ligi.

Klabu ya Real Madrid imejitoa katika mbio za kumsaini mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard baada ya klabu hiyo kuonekana kumuamini zaidi kinda Marco Asensio katika timu yao kwa sasa.

Inadaiwa kwamba klabu ya Arsenal imemuambia Jack Wilshaire asahau kuhusu kupewa mshahara mkubwa ndani ya klabu hiyo na sasa kiungo huyo ameanza kufikiria kuondoka hapo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here