Home Ligi Simba yatulizwa Zenj

Simba yatulizwa Zenj

2783
0
SHARE

Simba imebanwa na kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 ikicheza mechi ya kwanza Mapinduzi Cup 2017/18 dhidi ya Mwenge kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Jamal Mwambeleko alianza kuifungia Simba bao dakika ya pili (2) akiunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ lakini Mwenge walisawazisha dakika ya 28 goli likifungwa na Homoud Abrahman.

Kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya Mwenge kilisheheni wachezaji wengi ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Emanuel Mseja, Zimbwe Jr, Mlipili, Mwambeleko, Moses Kitandu, Said Ndemla.

Kocha wa Simba Masoud Djuma amesema matokeo hayo kwa namna nyingine yamechangiwa na uchovu wa safari ya kutoka Mtwara ambako walikwenda kucheza mechi ya ligi dhidi ya Ndanda.

“Tumetoka safari ya mbali kwa hiyo wachezaji walikuwa na uchovu ndio maana kipindi cha kwanza niliwapumzisha wachezaji wengi kwa sababu walikuwa na mchoko. Tumeyapokea matokeo tunaenda kujiandaa kwa ajili ya mchezo ujao”-Masoud Juma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here