Home Dauda TV Video: Msamaha anaoulilia Juma Mahadhi Yanga

Video: Msamaha anaoulilia Juma Mahadhi Yanga

6391
0
SHARE

Kama unakumbuka leo January 2, 2018 mchana kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiomba radhi kwa mashabiki, viongozi pamoja na benchi la ufundi la klabu yake.

Usiku wa siku hiyohiyo (saa 2:15 usiku) alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kilichoiwakilisha Yanga kwenye mechi ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, jambo jema ni kwamba Mahadhi aakatupia magoli mawili na kuiwezesha timu yake kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mlanege.

Baada ya mechi Mahadhi akazungumza na waandishi wa habari kueleza sababu iliyomfanya aombe radhi wadau wa Yanga pamoja na kushangilia goli lake la kwanza huku akiwa amepiga magoti. Dauda TV imekita kambi Zanzibar kufuatilia mashindano ya kombe la Mapinduzi, hapa chini kuna video ya kile alichozungumza Mahadhi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here