Home Ligi EPL Mourinho kuifikia rekodi mbovu ya LVG leo?

Mourinho kuifikia rekodi mbovu ya LVG leo?

6223
0
SHARE

United leo wanaufungua mwaka kwa kuwatembelea Everton ambapo michezo 6 iliyopita kati ya timu hizi mbili Manchester United hawajawahi kupoteza, wameshinda mechi nne na kupata suluhu mara mbili.

Mwezi April mwaka 2015 ilikuwa mara ya mwisho kwa Everton kuwapiga Manchester United ambapo siku hii Everton waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 0 mbele ya mashetani wekundu .

Lakini pamoja na hali halisi kwamba Everton wamekuwa wakipigwa sana na United ila katika michezo 5 iliyopita Goodison Park wamepoteza mchezo mmoja tu mbele ya United huku michezo mitatu wakishinda.

Siku za hivi karibuni Goodison Park pamekuwa sehemu ngumu sana kwa wapinzani wa Everton katika michezo 5 iliyopita hawajapoteza hata mchezo mmoja huku wakishinda michezo 4 kati ya 5.

Manchester United wanakwenda Goodison Park huku mchezo wao wa mwisho kumaliza bila kuruhusu bao ugenini ilikuwa ni mwezi October mwaka jana walipotoka sare ya bila bila na Liverpool.

Tayari mechi 4 zilizopita Manchester United hawajapata ushindi na kama hii leo tena wakishindwa kupata ushindi baasi Mourinho atakuwa ameifikia rekodi mbovu ya Louis Van Gaal ya December 2015 kucheza mechi 5 bila ushindi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here