Home Kimataifa Tarehe 5 nisizoweza kusahau kwa mwaka 2017, ni ipi wewe huwezi sahau?

Tarehe 5 nisizoweza kusahau kwa mwaka 2017, ni ipi wewe huwezi sahau?

8424
0
SHARE

Tarehe 5 June. Ilikuwa ni kilio na simanzi siku hii, Cheikh Tiote alifariki akiwa na miaka 30. Binafsi nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Tiote wakati akiwa yuko EPL pale Newcastle na tukio baya zaidi kwa upande wangu katika soka kwa mwaka huu.

Tarehe 8 March. Soka ni mchezo wa ajabu, PSG waliwatembelea Barca siku hii wakiwa na mtaji wa mabao 4 kwa 0 na kila mtu akawaza Barca anaaga Champions League. Mabao ya Lioneil Messi, Neymar, Suarez na Sergio yaliwashangaza PSG na mchezo ukaisha kwa bao 6 kwa 1, PSG wakaaga kwa aggregate ya 6 kwa 5.

Tarehe 26 August. Huu ulikuwa usiku wa kuelekea tarehe 27 na watu wengi tulikesha, kila mtu alikuwa na hamu kuona ni nini Floyd Money Mayweather anaweza kufanya mbele ya Conor McGregor na round ya 10 tu THE MONEY TEAM walishangilia baada ya Mayweather kushinda kwa TKO.

Tarehe 12 July. Inaweza ikawa inaonekana ajabu au sijui itaonekanaje lakini kwangu hii siku sitaisahau, nilipomuona live shujaa wangu Wayne Rooney, huu ulikuwa ujio wa klabu ya Everton nchini Tanzania na hakika hili nalo lipo kwenye kumbukumbu zangu mwaka huu.

Tarehe 10 October. Kila mtu alikata tamaa kumuona Lioneil Messi kombe la dunia, lakini alichofanya siku hii aliibeba Argentina mabegani na hat trick aliyopiga vs Ecuador iliwahakikishia Waargentina safari ya kwenda Urusi kwenye kombe la dunia mwakani

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here