Home Kitaifa Historia inavyoihukumu Ndanda kwa Simba

Historia inavyoihukumu Ndanda kwa Simba

3104
0
SHARE

Historia kwenye soka ni kitu muhimu sana hasa zile zinazohusu timu zinapokutana zenyewe kwa zenyewe au uso kwa uso ‘head to head’. Leo Juamosi December 30, 2017 Ndanda itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa 12.

Kuelekea mechi hiyo, Ndanda ina historia mbaya dhidi ya Simba huku kwa mnyama ikiwa ni tofauti, Simba kuifunga ndanda katika mechi za ligi ni kama vile kumsukuma mlevi au vija wa kisasa wanesema ‘utatembelea ganda la ndizi mlima kitonga’ yaani unatereza tu.

Historia inaonesha kwamba, katika mechi sita zilizopita zinazohusisha timu hizo, Simba imeshinda mechi, kila timu imecheza mechi tatu kwenye uwanja wa nyumbani na tatu nyingine ikiwa ugenini.

  • 18/12/2016 Ndanda 0-2 Simba
  • 20/08/0216 Simba 3-1 Ndanda
  • 10/03/ 2016 Simba 3-0 Ndanda
  • 01/01/2016 Ndanda 0-1 Simba
  • 25/04/2015 Simba 3-0 Ndanda
  • 17/01/2015 Ndanda 0-2 Simba

Simba bila Omog

Wachezaji watacheza kwa mara ya kwanza bila kocha wao mkuu ambaye ametimuliwa hivi karibuni baada ya Simba kuvuliwa ubingwa katika mechi za awali za kombe la shirikisho Tanzania bara kwa kufungwa na Green Warriors ya ligi daraja lapili, kwa sasa kikosi cha Simba kipo chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma ambaye atasimama kukiongoza kwa mara ya kwanza bila bosi wake.

Mbio za ubingwa 2017/18

Simba inapambana kuhakikisha inatwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo msimu wa 2011/12, imekuwa ni kiu yao kutwaa taji hilo ambalo wamelikosa kwa muda mrefu mfululizo huku watani zao Yanga wakiweka rekodi ya kulitwaa mara tatu mfululizo katika misimu ya hivi karibuni.

Ushindi wa jana wa Azam 3-0 Stand United umeitoa Simba kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi, ushindi pekee ndio utawarejesha tena kwenye nafasi hiyo. Endapo Simba itapoteza mchezo wao dhidi ya Ndanda, watatoa mwanya kwa Yanga kuwapiku katika nafasi ya pili endapo watashinda mechi yao ya kesho dhidi ya Mbao, kumbuka Simba na Yanga zinatofautiana kwa alama mbili pekee.

Baada ya mechi za mzunguko wa 12, ligi itasimama tena kupisha mashindano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, kila timu inayowania ubingwa inatamani kuona ipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kabla ya kwenda kwenye michuano ya Mapinduzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here