Home Ligi “Hatutaki kubebwa”-Haji Manara

“Hatutaki kubebwa”-Haji Manara

5395
0
SHARE

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema, hawataki timu yao ibebwe badala yake wanataka matokeo yote yapatikane uwanjani ili kupata bingwa halali na si aliyepangwa tangu awali.

Manara amesema Simba isipendelewe wala isinyimwe haki pale inapostahili na inapotokea kufungwa basi iwe kwa uhalali pia amelipongeza shirikisho la soka nchini TFF kwa kutoingilia masuala ya uwanjani.

“Sasa hivi TFF haiingilii masuala ya uwanjani hakuna maamuzi tata kila jambo linafanyika kwa weledi, sisi tulifungwa mchezo wa FA kuna baadhi ya watu walisema TFF hii itawabeba Simba, tumefungwa wala hakubebwa mtu kwa hiyo TFF hii imedhamiria kutenda haki na mimi nawapongeza”-Haji Manara.

“Furaha yangu mimi TFF watende haki asionewe Simba kwa sababu wewe ulikuwa kiongozi wa Yanga wala asipendelewe Simba kwa sababu wewe ulikuwa kiongozi wa Simba. Mpira uchezwe uwanjani tupate bingwa halali ndio nalo sisitiza hilo, naomba watanzania wanielewe hatutaki kubebwa tunataka tushinde kihalali ikibidi tufungwe kihalali kama tulivyofungwa na Green Warriors tumefungwa kihalali hajalalamika kiongozi yeyote wa Simba, mwanachama wala shabiki.”

“Sasa isitokee tena mambo yake ya nyuma watu kujifungia chumbani wanaamua huyu kacheza na kadi milioni wenyewe wanasema lazima washinde tu hii ni timu ya nyumbani, mpira ule sasa hivi haupo na niwatahadharishe wale wanaofikiri kila mwaka ni wa ngamia.”

“Niwatahadharishe wale wanaodhani kila mwaka ni mwaka wa Ngamia, kuna miaka inakuwa ya Simba, Tembo, kwa hiyo sio kwamba na zile mbeleko mwaka huu hazitakuwepo tunatarajia bingwa atapatikana kwa matokeo ya uwanjani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here