Home Kitaifa Yanga yamtuliza Kakolanya

Yanga yamtuliza Kakolanya

4109
0
SHARE

Klabu ya Yanga imekiri kuwa inadaiwa na golikipa Beno Kakolanya na ipo katika mchakato wa kuhakikisha inamaliza deni hilo pamoja na wachezaji wengine ambao wana madai tofauti.

Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema, Kakolanya hajapata stahiki zake kama ambavyo wachezaji wengine hawajapata lakini golikipa huyo aliyesajiliwa toka Tanzania Prisons bado ana mkataba na mabingwa hao wanaotetea taji la VPL.

“Kakolanya ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba wake, amepata stahiki zake kama wachezaji wengine ambavyo wamepata, hajapata stahiki zake kama wachezaji wengine ambavyo hawajapata , sasa inakuja ni namna gani mtu anaipokea hiyo hali na nani anazungumza naye. Klabu ikisema iweke wazi kila inachokifanya kwa wacheza nadhani haitakuwa sawa.”

“Yapo madai, hakuna taasisi ambayo haipitii changamoto madai. Suala la Beno tunalifahamu na litamalizika, kitu kizuri ni namna yeye anavyofikisha taarifa zake kwa sababu si kila mtu anaweza kupokea vizuri kile ambacho yeye anahisi ni sahihi.”

“Hayupo kwenye kikosi kwa sasa ana ruhusa mama yake ni mgonjwa anaendelea kumuuguza na taarifa tunapata kwa sababu tunawasiliana nae. Hakuna jambo tunaliacha linapita, tunawasiliana na wachezaji kila eneo ambalo wapo na tunawasaidia kila kadiri inavyowezekana.”

Suala la Beno Kakolanya kuidai Yanga pesa za usajili limekuwa likishika kasi kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii huku meneja wa mchezaji huyo Suleiman Haroub kutishia kulifikisha suala hilo TFF.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here