Home Ligi EPL Arsene Wenger aifikia rekodi ya Alex Ferguson na kumbukumbu kibao

Arsene Wenger aifikia rekodi ya Alex Ferguson na kumbukumbu kibao

4042
0
SHARE

Usiku wa leo katika mechi zidi ya Crystal Palace Arsene Wenger anaifikia rekodi ya Alex Ferguson ya kuwa kocha aliyeshiriki michezo mingi ya EPL 810, lakini Wenger ana kumbukumbu nyingi sana tangu aanze kuinoa Arsenal 1996.

Ilikuwa ni siku ya tarehe 12 October mwaka 1996 ambapo kocha Arsene Wenger alianza kukaa katika benchi la Arsenal katika mchezo zidi ya Blackburn Rovers ambao walishinda kwa mabao 2 kwa 1, lakini nini haswa Wenger anakumbuka?

Mechi ya kwanza(vs Blackburn), hii ilikuwa mwaka 1996 na Arsene Wenger anasema hawezi sahau hiyo siku kwani wachezaji wengi walionekana wadogo na aliogopa kuingia nao uwanjani lakini walishinda mchezo wake wa kwanza.

Usajili wa Henry 1999, “Siwezi kusema kwamba Henry alikuwa namba moja au mbili katika wachezaji wakali wa Arsenal, lakini usajili wake hakika ulikuwa mafanikio makubwa kwa klabh yetu”

Vipi kuhusu kuondoka kwa Henry 2007? “Alinifuata akaniambia sikia kocha tuna timu ya vijana na mimi nina miaka 31 nahitaji kushinda na kwa sasa naona ni bora kuondoka wakati hawa wengine wakiendelea kukua”.

United kuwasimamisha mwaka 2004 “Michezo 49 bila kufungwa lilikuwa jambo kubwa, United walicheza vizuri japo muamuzi hakuwa sawa sana lakini sisi pia tulicheza vizuri ila hatukuwa na bahati siku ile”

Wenger akizungumzia tukio la Ferguson kupigwa na Pizza alisema Fabregas alirusha Pizza katika korido za uwanja wa Old Traford lakini hakuwa na nia ya kumpiga mtu ila bahati mbaya ilimrukia Alex Ferguson.

Fainali ya Champions League mwaka 2001, Arsenal waliokuwa 10 walikufa kwa bao 2 kwa 1 mbele ya Barcelona na Wenger anakiri kwamba huo ndio wakati alioumia sana, kwani walikuwa na timu bora lakini walishindwa kucheza 11 zidi ya Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here